top of page

Lengo la Uumbaji

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Jul 31
  • 1 min read

ree

Kwa hiyo Mungu akamuumba mtu kwa mfano wake mwenyewe, kwa mfano wa Mungu alimuumba; mwanaume na mwanamke aliwaumba. (Mwanzo 1:27)


Mungu aliumba wanadamu kwa mfano wake ili ulimwengu ujae na wale wanaomuakisi Mungu. Mifano ya Mungu. Sanamu bilioni saba za Mungu. Ili kwamba hakuna mtu atakayekosa kuelewa lengo la uumbaji. 

 

Hakuna mtu (isipokuwa kama ni kipofu kabisa) anayeweza kukosa kuelewa lengo la ubinadamu, yaani, Mungu — kumjua, kumpenda, na kumdhihirisha Mungu. Malaika wanalia katika Isaya 6:3, “Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake!” Imejaa mabilioni ya watu wanaobeba sura ya Mungu. Magofu ya utukufu. 

 

Lakini si wanadamu tu. Asilia pia! Kwa nini tuishi katika ulimwengu wenye kustaajabisha namna hii? Kwa nini ulimwengu mkubwa hivyo?

 

Wakati fulani nilisoma kwamba kuna nyota nyingi zaidi katika ulimwengu kuliko maneno na sauti ambazo wanadamu wote wa wakati wote wamewahi kusema. Mbona zipo nyingi hivyo? Kubwa mno? Zenye mwangaza mkali sana? Katika umbali huo usiofikirika? Biblia iko wazi juu ya hili: “Mbingu zatangaza utukufu wa Mungu” (Zaburi 19:1).

 

Mtu akiuliza, “Ikiwa dunia ndiyo sayari pekee inayokaliwa na mwanadamu na ndiye mkaaji pekee mwenye busara kati ya nyota, kwa nini ulimwengu mkubwa hivyo na usio na kitu?” Jibu ni: Hili halihusiani na sisi. Inamuhusu Mungu. Na ni kauli isiyotosha. Yeye ni mtukufu zaidi. Mkuu zaidi katika nguvu. Mkuu zaidi katika upeo. Mwenye mwangaza zaidi. Kuliko yota na sayari zote zikiwekwa pamoja. Mtu mmoja mwenye hekima alisema, ulimwengu ni kama karanga ambayo Mungu huibeba mfukoni mwake.

 

Mungu alituumba ili tumjue na kumpenda na kumwonyesha. Na kisha akatupa dokezo la jinsi alivyo: ulimwengu.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page