Maana Ya Kumhimidi Bwana
- Dalvin Mwamakula
- Jul 31
- 1 min read

Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, na vyote vilivyo ndani yangu vilihimidi jina lake takatifu. (Zaburi 103:1)
Zaburi inaanza na kuisha na mtunga-zaburi akiihubiria nafsi yake imhimidi Bwana - "Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana" - na kuwahubiria malaika na majeshi ya mbinguni na kazi za mikono ya Mungu kwamba wanapaswa kufanya vivyo hivyo.
Mhimidini Bwana, enyi malaika zake, ninyi wenye nguvu mnaofanya neno lake, kutii sauti ya neno lake!Mhimidini Bwana, enyi majeshi yake yote, mawaziri wake, wanaofanya mapenzi yake!Mhimidini Bwana, enyi kazi zake zote, katika sehemu zote za utawala wake.Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana! (Zaburi 103:20-22)
Zaburi hii inazingatia sana kumhimidii Bwana. Je, inamaanisha nini kumhimdii Bwana?
Inamaanisha kuzungumza vyema kuhusu ukuu na wema wake — na kumaanisha kwa dhati kutoka ndani kabisa ya nafsi yako.
Kile ambacho Daudi anafanya katika mistari ya kwanza na ya mwisho ya zaburi hii, anaposema, “Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana,” ni kusema kwamba kuzungumza vizuri kuhusu wema na ukuu wa Mungu lazima utoke katika nafsi.
Kumbariki Mungu kwa kinywa bila roho itakuwa unafiki. Yesu alisema, “Watu hawa huniheshimu kwa midomo, lakini mioyo yao iko mbali nami” (Mathayo 15:8). Daudi anajua hatari hiyo, na anajihubiria mwenyewe. Anaiambia nafsi yake isiruhusu hili kutokea.
“Njoo, nafsi, utazame ukuu na wema wa Mungu. Ungana na kinywa changu, na tumbariki Bwana kwa uhai wetu wote. Nafsi, hatutakuwa wanafiki!”




Comments