Maana Ya Kumuombea Adui Yako
- Dalvin Mwamakula
- Mar 31
- 2 min read

"Wapendeni adui zenu na waombeeni wanaowatesa ninyi." (Mathayo 5:44)
Maombi kwa ajili ya adui zako ni mojawapo ya aina ya upendo mkuu, kwa sababu ina maana kwamba unatamani kwa dhati jambo zuri litokee kwao.
Unaweza kufanya mambo mazuri kwa ajili ya maadui zako bila kuwa na nia ya dhati kwamba mambo yawe mazuri kwao. Lakini maombi kwa ajili yao ni mbele za Mungu anayejua moyo wako, na maombi ni kuwaombea kwa Mungu kwa niaba yao.
Huenda ikawa ni kwa ajili ya uongofu wao. Huenda ikawa ni kwa ajili ya toba yao. Huenda wangeamshwa na uadui uliomo mioyoni mwao. Inawezekana kwamba watazuiliwa katika mzunguko wao wa dhambi, hata kama itachukua ugonjwa au janga kufanya hivyo. Lakini maombi ambayo Yesu anafikiria hapa ni kwa ajili ya mema yao daima.
Kuombea adui zako ni aina ya upendo mkuu, ukitamani mema, wokovu, na furaha yao ya milele.
Hivi ndivyo Yesu alivyofanya alipokuwa msalabani:
Baba, uwasamehe, kwa maana hawajui watendalo. (Luka 23:34)
Na ndivyo Stefano alivyofanya alipokuwa akipigwa mawe:
Akapiga magoti akalia kwa sauti kuu, "Bwana, usiwahesabie dhambi hii!" (Matendo 7:60)
Tumeitwa na Yesu sio tu kufanya mambo mema kwa adui zetu, kama vile kuwasalimu na kuwasaidia mahitaji yao (Mathayo 5:47); pia anatuita kutamani mema yao, na kueleza matamanio hayo katika maombi, hata wakati adui hayupo.
Mioyo yetu inapaswa kutamani wokovu wao na kutamani uwepo wao mbinguni pamoja nasi na kutamani furaha yao ya milele. Mungu atupe neema ya kuomba kama mtume Paulo alivyoomba kwa ajili ya Wayahudi, ambao wengi wao walifanya maisha yake kuwa magumu sana:
Tamanio la moyo wangu na maombi yangu kwa Mungu ni kwamba waokolewe. (Warumi 10:1)
ความคิดเห็น