top of page

Maana ya Ufufuo kwa ajili Yetu

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Jul 31
  • 1 min read
ree

Ukikiri kwa kinywa chako kwamba “Yesu ni Bwana,” na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka. (Warumi 10:9)


Inamaanisha nini “kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu”? Shetani anaamini kwamba Mungu alimfufua Yesu kutoka kwa wafu. Aliliona likitokea. Ili kujibu swali hilo, tunahitaji kutafakari ufufuo unamaana gani kwa watu wa Mungu.


Maana ya ufufuo ni kwamba Mungu yuko kwa ajili yetu. Anataka kuungana nasi. Analenga kuzishinda hisia zetu zote za kuachwa na kutengwa.


Ufufuo wa Yesu ni tamko la Mungu kwa Israeli na ulimwengu kwamba hatuwezi kujitahidi kwa njia zetu kuufikia utukufu, bali anataka kufanya yasiyowezekana kutufikisha huko .


Ufufuo ni ahadi ya Mungu kwamba wote wanaomwamini Yesu watakuwa wanufaika wa nguvu za Mungu za kutuongoza katika njia za haki na katika bonde la mauti.

Kwa hiyo, kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua Yesu kutoka kwa wafu ni zaidi ya kukubali ukweli. Inamaanisha kuwa na uhakika kwamba Mungu yuko upande wako, kwamba ameungana na wewe, kwamba anabadilisha maisha yako, na kwamba atakuokoa kwa ajili ya furaha ya milele.


Kuamini ufufuo kunamaanisha kuamini ahadi zote za maisha, tumaini, na haki ambazo ufufuo unawakilisha. 


Inamaanisha kuwa na uhakika sana juu ya nguvu na upendo wa Mungu kiasi kwamba hakuna hofu ya kupoteza vitu vya dunia au tamaa ya kupata mali ya dunia itakayotuvuta kutotii mapenzi yake. 


Hiyo ndiyo tofauti kati ya Shetani na watakatifu. Tunaomba, Mungu aitahiri mioyo yetu ili kumpenda (Kumbukumbu la Torati 30:6) na kupumzika katika ufufuo wa Mwana wake.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page