top of page

Maficho ya Wasiojiweza

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • May 29
  • 1 min read
ree

Tazama jinsi ulivyo tele wema wako, ambao ulionao. . . ukitenda kazi kwa ajili ya wale wakukimbiliao. (Zaburi 31:19)

 

Uzoefu wa neema ya wakati ujao mara nyingi hutegemea kama tutapata kimbilio kwa Mungu, au kama tunatilia shaka utunzaji wake na kukimbilia hifadhi pengine.

 

Kwa wale wanaomkimbilia Mungu, ahadi za neema ya wakati ujao ni nyingi na tele. 

 

  • Hakuna hata mmoja wa wale wanaokimbilia kwake atakayehukumiwa. (Zaburi 34:22

  • Yeye ni ngao kwa wote wanaomkimbilia. (2 Samweli 22:31

  • Heri wote wanaomkimbilia. (Zaburi 2:12

  • Bwana ni mwema, ni ngome siku ya taabu; anawajua wale wanaomkimbilia. (Nahumu 1:7

 

Hatupati wala kustahili kitu chochote kwa kukimbilia kwa Mungu. Kujificha, kwa sababu sisi ni dhaifu na tunahitaji ulinzi, sio kazi ya kupongeza utoshelevu wetu binafsi. Inachofanya tu ni kuonyesha kwamba tunajiona kuwa wanyonge na mahali pa kujificha kama mahali pa uokoaji. 

 

Katika ahadi hizo zote nilizozinukuu, shariti la baraka kubwa kutoka kwa Mungu ni kwamba tukimbilie kwake. Hali hiyo sio ya kustahiki; ni hali ya kukata tamaa na kukiri udhaifu na hitaji na uaminifu. 

 

Kukata tamaa hakuombi kwa madai wala kustahili; huomba rehema na kutazamia neema.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page