top of page

Makusudi ya Mungu Katika Njia Zisizonyooka

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Apr 28
  • 2 min read

Updated: May 1

Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye. (Wakolosai 3:17)

 

Umewahi kujiuliza Mungu anafanya nini unapo kuwa unatafuta kitu ulichopoteza mahala ambapo sio sahihi na unakihitaji sana? Yeye anajua mahali kilipo, na bado anakuruhusu utafute mahala ambapo sio.

 

Wakati fulani nilihitaji nukuu kwa toleo jipya la kitabu changu Desiring God [Kuwa na Shauku na Mungu]. Nilijua nilikuwa nimeisoma katika kitabu cha Richard Wurmbrand. Nilifikiri ilikuwa katika kitabu chake cha ibada, Reaching Toward the Heights [Kufikia Viwango vya Juu]. Nilikuwa kama vile nakiona kwenye upande wa kulia wa kurasa zinazotazamana. Lakini sikuweza kuipata.


Lakini nilipokuwa nikitafuta, nilivutiwa kwenye nukuu yake ya Novemba 30. Nilipoisoma, nilisema, “Hii ndiyo sababu Bwana aliniruhusu niendelee kutafuta nukuu yangu mahali ’ambapo sio sahihi.” Hapa kulikuwa na hadithi iliyoonyesha kikamilifu kwamba hakuna kitu kinachoharibika tunachokifanya kwa jina la Yesu - hakuna chochote, hata kutafuta nukuu mahala ambapo sio sahihi. Hiki ndicho nilichosoma:

 

Katika nyumba ya watoto waliodumaa, Catherine alilelewa kwa miaka ishirini. Mtoto huyo alikuwa [amelemaa kiakili] tangu mwanzo, na hakuwahi kusema neno lolote, bali alipewa mboga mboga tu. Ama alitazama kuta kimya kimya au kufanya harakati zizizo na maana. Kula, kunywa, kulala, yalikuwa maisha yake yote. Alionekana kutoshiriki hata kidogo katika kile kilichotokea karibu naye. Mguu ilibidi ukatwe. Wafanyakazi walimtakia Cathy heri na walitumaini kwamba Bwana angelimtwaa hivi karibuni kwake.


Siku moja daktari alimwita mkurugenzi aje haraka. Catherine alikuwa anakufa. Wote wawili walipoingia chumbani, hawakuamini hisia zao. Catherine alikuwa akiimba nyimbo za masikitiko alizosikia na kuzifuhamu, zile tu zinazofaa kwa vitanda vya mauti. Alirudia tena na tena wimbo wa Wajerumani, "Nafsi hupata wapi nchi ya baba, pumziko lake?" Aliimba kwa muda wa nusu saa na uso uliobadilika, kisha akaaga dunia kimya kimya. (Imechukuliwa kutoka kwa The Best Is Still to Come, Wuppertal: Sonne und Shild)

 

Je, jambo lolote linalofanywa kwa jina la Kristo linaweza kupotea bure?

 

Utafutaji wangu uliofadhaika, usio na maana wa kutafuta kile nilichofikiri nilikihitaji haukupotezwa. Kumwimbia mtoto huyu mlemavu hakukupotea bure. Na uchungu wako, kupangwa sio kupoteza - sio ikiwa unamtazamia Bwana kwa kazi yake isiyotarajiwa, na kufanya kila kitu kwa jina lake (Wakolosai 3:17).

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page