Malipo ya Uvumilivu
- Dalvin Mwamakula
- Apr 28
- 2 min read
Updated: May 1

“Nanyi mlikusudia mabaya juu yangu, lakini Mungu alikusudia kwa ajili ya mema, ili kwamba watu wengi wahifadhiwe hai.” (Mwanzo 50:20)
Hadithi ya Yusufu katika Mwanzo 37–50 ni somo kuu kwa nini tunapaswa kuwa na imani katika neema ya Mungu mwenyenzi ya wakati ujao.
Yusufu anauzwa utumwani na ndugu zake, jambo ambalo lazima lilijaribu sana uvumilivu yake. Lakini anapewa kazi nzuri katika nyumba ya Potifa huko Misri. Kisha, anapotenda kwa unyoofu mahali pa utii pasipo pangwa, mke wa Potifa husema uwongo kuhusu uadilifu wake na kumfanya atupwe gerezani—jaribio jingine kubwa la uvumilivu wake.
Lakini tena mambo yanakuwa mazuri, na mlinzi wa gereza anampa wajibu na heshima. Lakini wakati tu anapofikiri kwamba anakaribia kupata ahueni kutoka kwa mnyweshaji wa Farao, ambaye alimtafsiria ndoto yake, mnyweshaji anamsahau kwa miaka miwili zaidi. Jaribio jingine chungu kwa uvumilivu wake.
Hadithi ya Yusufu inatufundisha kuwa na imani katika neema ya Mungu kwa siku zijazo
Hatimaye, maana ya mikengeuko yote hii na ucheleweshaji inakuwa wazi. Yusufu anainuliwa kuwa kiongozi wa Misri, wa pili baada ya Farao. Anaishia kuokoa kutokana na njaa ndugu wale wale waliomuuza utumwani. Yusufu anawaambia ndugu zake ambao wameachana nao kwa muda mrefu, “Mungu alinituma mbele yenu ili kuwahifadhia mabaki duniani, na kuwahifadhi hai kwa ajili yenu wengi. . . . Nanyi mlikusudia mabaya juu yangu, lakini Mungu alikusudia kuwa jema, ili watu wengi wahifadhiwe hai” (Mwanzo 45:7;50:20).
Ni nini kingekuwa ufunguo wa uvumilivu kwa Yusufu katika miaka hiyo yote mirefu ya uhamishoni na kunyanyaswa? Jibu ni: imani katika enzi kuu ya Mungu, neema ya wakati ujao - neema kuu ya Mungu ya kugeuza mahali pasipopangwa na mwendo usiopangwa kuwa mwisho wa furaha zaidi unaowezekana.
Huo ndio ufunguo wa uvumilivu wetu pia. Je, tunaamini kwamba Mungu anafanya kazi kwa ajili yetu katika namna ya ajabu na zenye uchungu zaidi za maisha yetu?
Comments