top of page

Mambo Sita Yanayomaanisha Kuwa Ndani Ya Kristo Yesu

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Jul 31
  • 2 min read
ree

[Mungu] ambaye alituokoa na kutuita katika mwito mtakatifu: si kwa kadiri ya matendo yetu mema bali kwa sababu ya kusudi lake mwenyewe na neema yake. Neema hii tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele.  (2 Timotheo 1:9)


Kuwa "ndani ya Kristo Yesu" ni ukweli wa ajabu. Inafurahisha sana kuunganishwa na Kristo. Kufungamanishwa na Kristo. 

 

Ikiwa uko “ndani ya Kristo” sikiliza maana yake kwako:

 

  1. Katika Kristo Yesu ulipewa neema kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu. 2 Timotheo 1:9, “Naye alitupa neema katika Kristo Yesu kabla ya nyakati.

  2. Katika Kristo Yesu mlichaguliwa na Mungu kabla ya kuumbwa. Waefeso 1:4, “[Mungu] alituchagua katika [Kristo] kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.”

  3. Katika Kristo Yesu unapendwa na Mungu kwa upendo usioweza kutenganishwa. Warumi 8:38-39 , “Ninajua hakika ya kwamba, si mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kuwatenganisha watu kutoka katika upendo wa Mungu katika Kristo Yesu Bwana wetu.”

  4. Katika Kristo Yesu umekombolewa na kusamehewa dhambi zako zote. Waefeso 1:7, “ Katika [Kristo] tuna ukombozi kwa damu yake, msamaha wa makosa yetu.”

  5. Katika Kristo Yesu umehesabiwa haki mbele za Mungu na haki ya Mungu katika Kristo inahesabiwa kwako. Wakorintho wa pili 5:21 , “Kwa ajili yetu [Mungu] alimfanya [Kristo] kuwa dhambi yeye asiyejua dhambi, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye.”

  6. Katika Kristo Yesu umekuwa kiumbe kipya na mwana wa Mungu. Wakorintho wa pili 5:17, “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya. Ya kale yamepita; tazama, yamekuwa mapya.” Wagalatia 3:26, " Katika Kristo Yesu ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani."

 

Ninaomba kwamba kamwe usichoke kuchunguza na kushangilia upendeleo usiokwisha wa kuwa “ndani ya Kristo Yesu.”

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page