top of page

Maneno ya Kupambana

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Nov 12
  • 2 min read
ree

Usiogope, kwa maana mimi niko pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; Nitakutia nguvu, nitakusaidia, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu. (Isaya 41:10)

 

Ninapokuwa na wasiwasi kuhusu mradi mpya hatari au mkutano, mimi hupambana na kutoamini na mojawapo ya ahadi zangu ninazotumia mara nyingi zaidi: Isaya 41:10.

 

Siku nilipoondoka kwa miaka mitatu kwenda kusoma Ujerumani, baba yangu alinipigia simu umbali mrefu huko New York na kunipa ahadi ya mstari huu kwenye simu.


Kwa miaka mitatu, nilinukuu mstari huu mara mamia ili kunipitisha katika vipindi vya mfadhaiko mkubwa. 

 

Wakati injini ya akili yangu iko katika hali ya kawaida, sauti ya gia ni sauti ya Isaya 41:10. Ninaupenda mstari huu.

 

Bila shaka, si mshale pekee nilionao katika ghala la hifadhi la silaha za vita vya imani yangu.

 

Ninapokuwa na wasiwasi kuhusu huduma yangu kutokuwa na maana na utupu, ninapigana na kutokuamini kwa ahadi ya Isaya 55:11, “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza kusudi langu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.”

 

Wakati nina wasiwasi juu ya kuwa dhaifu sana kufanya kazi yangu, ninapigana na kutokuamini kwa ahadi ya Kristo, "Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hukamilishwa katika udhaifu" (2 Wakorintho 12:9).

 

Ninapokuwa na wasiwasi juu ya maamuzi ninayopaswa kufanya kuhusu wakati ujao, ninapambana na kutokuamini kwa ahadi, “Nitakufundisha na kukuonyesha njia unayopaswa kuiendea; nitakushauri, jicho langu likikutazama” (Zaburi 32:8).

 

Ninapokuwa na wasiwasi kuwakabili wapinzani, ninapambana na kutoamini kwa ahadi, “Ikiwa Mungu yuko upande wetu, ni nani aliye juu yetu?” (Warumi 8:31).

 

Ninapokuwa na wasiwasi hali njema ya wale ninaowapenda, ninapambana na kutokuamini kwa ahadi ya kwamba ikiwa mimi, ambaye ni mwovu, najua jinsi ya kuwapa watoto wangu mambo mema, “si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao!” (Mathayo 7:11).

 

Basi kwa njia zote pigana na kutoamini kwa kila ahadi ndani ya kitabu. Lakini inasaidia kuwa na silaha moja abayo ndio kiini, silaha ya msingi. Na kwangu mimi hiyo imekuwa Isaya 41:10, “Usiogope, kwa maana mimi niko pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; Nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.” Ahadi ya thamani, ya thamani sana!

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page