Mateso Yanayoimarisha Imani
- Dalvin Mwamakula
- Jun 30
- 2 min read

Ndugu zangu, hesabuni kuwa ni furaha tupu mnapopatwa na majaribu mbalimbali, kwa sababu mnajua ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. (Yakobo 1:2-3)
Ingawa inaweza kuonekana kuwa ya ajabu,
kusudi moja yapo la kutikiswa na kuteseka ni kufanya imani zetu zisitikisike zaidi.
Imani ni kama tishu za misuli: ukiiwekea mkazo hadi kikomo, inakuwa na nguvu, sio dhaifu. Hichi ndicho anachomaanisha Yakobo hapa. Imani yako inapotishwa na kujaribiwa na kunyooshwa hadi kufikia kiwango cha kuvunjwa, matokeo yake ni uwezo mkubwa wa kustahimili. Anauita uthabiti.
Mungu anapenda imani sana kiasi kwamba ataijaribu hadi sehemu ya kuvunjika ili kuiweka safi na yenye nguvu. Kwa mfano, alifanya hivi kwa Paulo kulingana na 2 Wakorintho 1:8-9,
Ndugu wapendwa, hatutaki mkose kujua kuhusu zile taabu tulizopata huko Asia. Kwa maana tulilemewa na mizigo sana, kiasi cha kushindwa kuvumilia, hata tulikata tamaa ya kuishi. Kwa kweli, mioyoni mwetu tulihisi tumekabiliwa na hukumu ya kifo, ili tusijitegemee sisi wenyewe bali tumtegemee Mungu afufuaye wafu.
Neno “ili” linaonyesha kwamba kulikuwa na kusudi katika mateso haya ya kupita kiasi: ilikuwa ili kwamba—kwa kusudi kuwa —Paulo asijitegemee yeye mwenyewe na rasilimali zake, bali Mungu—hasa neema iliyoahidiwa ya Mungu katika kufufua wafu.
Mungu anathamini sana imani yetu ya moyo wote kiasi kwamba, kwa neema, ikiwa ni lazima, ataondoa kila kitu kingine katika ulimwengu tunachoweza kujaribiwa kutegemea - hata maisha yenyewe. Kusudi lake ni kwamba tukue zaidi na zaidi katika imani yetu kwamba yeye mwenyewe atakuwa yote tunayohitaji.
Anataka tuweze kusema pamoja na mtunga zaburi, “Nina nani mbinguni ila wewe? Na hakuna kitu ninachotamani duniani isipokuwa wewe. Mwili wangu na moyo wangu vinaweza kupunguka, lakini Mungu ni ngome ya moyo wangu na sehemu yangu milele” (Zaburi 73:25–26).
Comments