top of page

Mbinu Kumi na Tano za Furaha

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Mar 31
  • 2 min read
ree

Umenijulisha njia ya uzima; utanijaza na furaha mbele zako; pamoja na furaha za milele katika mkono wako wa kuume. (Zaburi 16:11)

 

Katika maisha haya ya dhambi na maumivu, furaha ipo vitani. Kama imani tu. Na Paulo anamwambia Timotheo, “Pigana vile vita vizuri vya imani” (1 Timotheo 6:12). Ndivyo ilivyo kwa furaha. Lazima tuifanyie kazi na kuipigania. Paulo aliwaambia Wakorintho, “Tunafanya kazi pamoja nanyi kwa furaha yenu” (2 Wakorintho 1:24).


Katika maisha haya ya dhambi na maumivu, furaha inahitaji kupiganiwa kama imani. Paulo anamwambia Timotheo, “Pigana vile vita vizuri vya imani”.

 

Tutawezaje basi kupigania furaha? Hapa kuna vidokezo 15.

 

  1. Tambua kwamba furaha ya kweli katika Mungu ni zawadi.

  2. Tambua kwamba shangwe lazima ipigwe vita bila kukoma. Na usikatishwe tamaa na kitendawili cha vidokezo hivi viwili vya kwanza!

  3. Azimia kushambulia dhambi zote zinazojulikana maishani mwako, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

  4. Jifunze siri ya hatia yenye ujasiri — jinsi ya kupigana kama mwenye dhambi aliyehesabiwa haki.

  5. Tambua kwamba vita kimsingi ni vita ya kuona - kumwona Mungu jinsi alivyo.

  6. Tafakari neno la Mungu mchana na usiku.

  7. Omba kwa bidii na daima kwa ajili ya kufunguliwa macho ya moyo na mwelekeo kwa ajili ya Mungu.

  8. Jifunze kujihubiria kuliko kujisikiliza mwenyewe.

  9. Tumia muda na watu waliojawa Mungu ambao wanakusaidia kumwona Mungu na kupigana vita.

  10. Kuwa na uvumilive katika usiku ambao Mungu anaonekana hayupo.

  11. Pata mapumziko, mazoezi, na mlo unaofaa ambao mwili wako ulitengenezwa na Mungu uwe navyo.

  12. Tumia ipasavyo ufunuo wa Mungu katika asili - tembea msituni.

  13. Soma vitabu vizuri kuhusu Mungu na wasifu wa watakatifu wakuu.

  14. Fanya jambo gumu na la upendo kwa ajili ya wengine (ushahidi wako wa maneno na matendo ya rehema).

  15. Pata maono ya kimataifa kwa ajili ya Kristo, na ujitoe kwa wale ambao hawajafikiwa.

 

Kila moja ya hizo ina mistari ya Biblia ya kuiunga mkono. Ukitaka kuiona, ipo katika kitabu 'When I Don’t Desire God: How to Fight for Joy'.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page