top of page

Mfanye Shetani Ajue Kushindwa Kwake

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Mar 31
  • 2 min read
ree

Mpingeni shetani naye atawakimbia. (Yakobo 4:7)


Kadri Shetani anavyoonekana kuwa halisi katika siku zetu — na kadri anavyoonekana kuwa na shughuli nyingi — ndivyo ushindi wa Kristo unavyokuwa wa thamani zaidi kwa wale wanaomwamini.

 

Agano Jipya linafundisha kwamba Kristo alipokufa na kufufuka tena, Shetani alishindwa kabisa. Amepewa muda mdogo wenye mipaka, lakini nguvu zake dhidi ya watu wa Mungu zinavunjwa na uharibifu wake ni hakika.

 

  • "Kwa kusudi hiyo Mwana wa Mungu alidhihirishwa ili kuziharibu kazi za Ibilisi." (1 Yohana 3:8)

  • “[Kristo] naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo [mwili na damu], ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi.” (Waebrania 2:14)

  • “[Mungu] aliwapokonya silaha watawala na wenye mamlaka na kuwafedhehesha waziwazi, kwa ushindi katika yeye.” (Wakolosai 2:15)

 

Agano Jipya linafundisha kwamba kifo na ufufuo wa Kristo vilimshinda Shetani kabisa, na nguvu zake dhidi ya watu wa Mungu zimevunjwa.

Kwa maneno mengine, pigo kuu lilipigwa pale Kalvari. Na siku moja, uhuru wa Shetani wenye mipaka utakwisha, Ufunuo 20:10 husema, “Ibilisi . . . [atatupwa] ndani ya ziwa la moto . . . naye atateswa mchana na usiku hata milele na milele.”

 

Je, hii ina maana gani kwetu sisi tunaomfuata Yesu Kristo?

 

  • "Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu." (Warumi 8:1)

  • “Ni nani atakayewashtaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye anayehesabia haki!” (Warumi 8:33)

  • “[Wala] malaika, wala watawala, wala mambo yaliyopo wala yatakayokuja, wala nguvu, wala kimo, wala kina, wala cho chote kilicho katika uumbaji wote, hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.” (Warumi 8:38-39)

  • "Aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia." (1 Yohana 4:4)

  • “Nao [watakatifu] wamemshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo na kwa neno la ushuhuda wao.” (Ufunuo 12:11)

 

Kwa hiyo, “Mpingeni Ibilisi, naye atawakimbia! Ameshindwa, na sisi tumepewa ushindi. Kazi yetu sasa ni kuishi katika ushindi huo na kumfanya Shetani ajue kushindwa kwake.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page