Mji Mzuri
- Dalvin Mwamakula
- Jan 27
- 1 min read

Amewaandalia mji. (Waebrania 11:16)
Hakuna uchafuzi wa mazingira, hakuna grafiti, takataka, hakuna rangi inliyochubuka au gereji zinazooza, hakuna nyasi iliyokufa au chupa zilizovunjika, hakuna mazungumzo makali ya mitaani, hakuna makabiliano ya usoni, hakuna mizozo ya nyumbani au vurugu, hakuna hatari usiku, hakuna uchomaji moto, au kusema uwongo au kuiba au kuua, hakuna uharibifu, na hakuna ubaya.
Mji wa Mungu utakuwa mkamilifu, kwa sababu Mungu atakuwa ndani yake. Atatembea ndani yake na kuzungumza ndani yake na kujidhihirisha katika kila sehemu yake. Yote ambayo ni mema na mazuri na takatifu na ya amani na ya kweli na ya furaha yatakuwa pale, kwa sababu Mungu atakuwa huko.
Mji wa Mungu utakuwa mkamilifu na utajawa na mema, matakatifu, mazuri, amani, kweli, na furaha kwasababu ya Uwepo wa Mungu.
Haki kamilifu itakuwepo na italipa mara elfu kwa kila maumivu yaliyopatikana kwa kumtii Kristo katika ulimwengu huu. Na hautaharibika kamwe. Kwa hakika, utang'aa zaidi na zaidi kadiri umilele unavyoenea hadi katika enzi zisizokoma za furaha inayoongezeka.
Unapotamani mji huu kuliko vitu vingine vyote duniani, basi unamheshimu Mungu, ambaye, kulingana na Waebrania 11:10, ndiye mbunifu na mjenzi wa jiji hilo. Na Mungu anapoheshimiwa, hupendezwa na haoni haya kuitwa Mungu wako.




Comments