top of page

Mpe Mungu Kisasi Chako

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Jun 30
  • 2 min read
ree

Wapendwa, msilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Ni juu yangu kulipiza kisasi; mimi nitalipiza, asema Bwana. (Warumi 12:19)

 

Kwa nini hii ni ahadi muhimu sana katika kushinda mwelekeo wetu wa uchungu na kisasi? Sababu ni kwamba ahadi hii inajibu moja ya msukumo wenye nguvu zaidi nyuma ya hasira - msukumo ambao sio kosa kabisa.

 

Katika visa vingi, makosa ya kweli yamefanywa kwetu. Kwa hiyo, sio vibaya kabisa kuhisi kwamba haki inapaswa kutendeka. Ubaya ni kuhisi kwamba ni lazima tufanye jambo hilo litendeke na kwamba tunaweza kuhisi uchungu mpaka litimie. Hili litakuwa kosa baya sana.

 

Wakati wa siku zangu za seminari, mimi na Noël tulikuwa katika kikundi kidogo cha wanandoa ambao walianza kuhusiana kwa kina baina yao. Jioni moja tulikuwa tukijadili msamaha na hasira. Mke mmoja mdogo baina yao alisema kwamba asingeweza na hatoweza kumsemehe mama yake kwa jambo ambalo alimfanyia alipokuwa msichana mdogo.

 

Tulizungumza kuhusu baadhi ya amri za kibiblia na maonyo kuhusu roho ya kutosamehe.


  • Kuweni wafadhili na wenye kuhurumiana ninyi kwa ninyi, mkisameheana ninyi kwa ninyi kama vile naye Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi. (Waefeso 4:32)


  • Lakini msipowasamehe watu wengine makosa yao, naye Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu. (Mathayo 6:15)

 

Tunaweza kuwa na uhakika kwamba makosa yote yatashughulikiwa na Mungu na kwamba tunaweza kuyaacha mikononi mwake kwa sababu kisasi ni cha Bwana.

Lakini yeye hakutaka kubadilika. Kwa hiyo nilimwonya kwamba nafsi yake ilikuwa hatarini ikiwa angeendelea na mtazamo huo wa uchungu usio na msamaha. Lakini alisisitiza kwamba hatamsamehe mama yake.

 

Neema ya hukumu ya Mungu imeahidiwa kwetu hapa katika Warumi 12 kama njia ya kutusaidia kushinda roho hiyo mbaya ya kisasi na uchungu.

 

Hoja ya Paulo ni kwamba tunaweza kuwa na uhakika kwamba makosa yote yatashughulikiwa na Mungu na kwamba tunaweza kuacha jambo hilo mikononi mwake kwa sababu kisasi ni cha Bwana. Ili kutupa motisha sisi kuweka tamaa zetu za kulipiza kisasi anatupa ahadi: “Mimi nitalipiza, asema Bwana.”

 

Ahadi inayotuweka huru kutokana na roho ya kutosamehe, uchungu, na ya kulipiza kisasi ni ahadi kwamba Mungu ataweka hesabu zetu sawa. Atafanya hivyo kwa haki zaidi na kwa rehema na kwa ukamilifu zaidi kuliko tunavyoweza kufanya. Anaadhibu dhambi zote. Hakuna mtu yeyote atakayeepuka kwa chochote. Anaiadhibu ama katika Kristo msalabani kwa wale wanaotubu na kumwamini, au jehanamu kwa wale wasiomtumaini. Kwa hiyo, tunaweza kusimama mbali na kumwachia Mungu nafasi ya kufanya kazi yake kamilifu.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page