Msaada wa Mbingu katika Ghadhabu Inayokuja
- Dalvin Mwamakula
- May 29
- 2 min read

Mungu anaona kuwa ni haki kuwalipa dhiki wale wanaowatesa nyinyi, na kuwapa nafuu nyinyi wenye dhiki. . . wakati Bwana Yesu atakapofunuliwa kutoka mbinguni pamoja na malaika zake wenye nguvu katika mwali wa moto, akiwalipiza kisasi wale wasiomjua Mungu na wale wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu. (2 Wathesalonike 1:6–8)
Itafika wakati uvumilivu wa Mungu utaisha. Wakati Mungu ameona watu wake wakiteseka kwa wakati uliowekwa, na hesabu iliyowekwa ya wafia imani imekamilika (Ufunuo 6:11), basi kisasi cha haki na takatifu kitakuja kutoka mbinguni.
Ona kwamba kisasi cha Mungu juu ya wale ambao wamewatesa watu wake ni “unafuu” kwetu. “Mwenyezi Mungu anaona kuwa ni haki kuwalipa dhiki wale wanaowatesa nyinyi, na kuwapa nafuu nyinyi mnao dhiki.” Kwa maneno mengine, hukumu kwa “wale wanaotutesa” ni aina ya neema kwetu.
Labda picha ya ajabu zaidi ya hukumu kama neema ni picha ya kuangamizwa kwa Babeli katika Ufunuo 18. Wakati wa kuangamizwa kwake, sauti kuu kutoka mbinguni inalia, “Furahini juu yake, enyi mbingu, nanyi watakatifu na mitume na manabii, kwa maana Mungu ametoa hukumu kwa ajili yenu juu yake.” (Ufunuo 18:20). Kisha umati mkubwa unasikika ukisema, “Haleluya! Wokovu na utukufu na nguvu ni vya Mungu wetu, kwa maana hukumu zake ni za kweli na za haki; kwa maana amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeiharibu dunia kwa uasherati wake, na kuipatia kisasi damu ya watumwa wake” (Ufunuo 19:1–2).
Itafika wakati uvumilivu wa Mungu utaisha
Wakati uvumilivu wa Mungu umemaliza mwendo wake wa ustahimilivu, na enzi hii imekwisha, na hukumu inakuja juu ya maadui wa watu wa Mungu, watakatifu hawatakataa haki ya Mungu.
Hilo lamaanisha kwamba maangamizo ya mwisho ya wale wasiotubu hayatakuwa taabu kwa watu wa Mungu.
Kutokuwa tayari kwa wengine kutubu hakutashikilia mapenzi ya watakatifu kuwa mateka. Kuzimu haitaweza kuitia mbingu katika taabu. Hukumu ya Mungu itakubaliwa, na watakatifu watapata uthibitisho wa ukweli kama neema kuu.




Comments