top of page

Msingi wa Hakikisho Lako

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Apr 28
  • 2 min read

Updated: May 1

ree

Mungu alikuchagua wewe kuwa limbuko la kwanza la kuokolewa, kwa kutakaswa na Roho. (2 Wathesalonike 2:13)

 

Biblia inazungumza juu ya kuchaguliwa kwetu—kuchaguliwa na Mungu—katika Kristo kabla ya kuwekwa misingi ya dunia (Waefeso 1:4) kabla hatujafanya lolote jema au baya (Warumi 9:11). Kwa hiyo, uchaguzi wetu hauna masharti kwa mantiki ya ndani zaidi. Sio imani yetu wala utii wetu ndio msingi wake. Ni bure na hatustahili kabisa.

 

Kwa upande mwingine, vifungu vingi katika Biblia huzungumzia wokovu wetu wa mwisho (tofauti na uteule wetu kabla ya milele) kuwa na masharti—yaani, unategemea mabadiliko ya moyo na maisha. Kwa hiyo, swali lazuka, Je, ninawezaje kuwa na uhakika kwamba nitadumu katika imani na utakatifu unaohitajika ili kuurithi uzima wa milele?

 

Jibu ni kwamba hakikisho limejikita katika uteule wetu. 2 Petro 1:10 inasema, “Fanyeni bidii zaidi kuuthibitisha wito wenu na uteule wenu , kwa maana mkizitenda hizo hamtaanguka kamwe. Uteuzi wa Kimungu ndio msingi wa ahadi ya Mungu ya kuniokoa, na kwa hiyo kwamba atafanya kazi ndani yangu kwa neema ya kutakasa kile ambacho neema yake ya kuchagua imeanza.

 

Hii ndiyo maana ya agano jipya. Kila mtu anayemwamini Yesu ni mnufaika wa usalama wa agano jipya, kwa sababu Yesu alisema katika Luka 22:20, “Kikombe hiki kinachomwagika kwa ajili yenu ni agano jipya katika damu yangu.” Yaani kwa damu yangu ninaweka agano jipya kwa wote walio wangu.

 

Katika agano jipya Mungu haamrishi utii; anautoa. “BWANA, Mungu wako, atautahiri moyo wako, na moyo wa uzao wako, ili kwamba umpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa nafsi yako yote, upate kuishi” (Kumbukumbu la Torati 30:6). “Nitatia roho yangu ndani yako, na kukusababisha kutembea katika sheria zangu” (Ezekieli 36:27; taz. 11:20). Hizo ni ahadi za agano jipya.

 

Uchaguzi ni kujitolea wa milele wa Mungu kufanya hivyo kwa ajili ya watu wake. Kwa hiyo, uchaguzi unahakikisha kwamba wale ambao Mungu huwahesabia haki kwa imani bila shaka atawatukuza (Warumi 8:30). Hii ina maana kwamba bila kushindwa atafanya kazi ndani yetu masharti yote yaliyowekwa kwa ajili ya utukufu.

 

Uteule ndio msingi wa mwisho wa hakikisho letu kwa sababu, ni dhamira yake Mungu kuokoa, pia ni dhamira yake Mungu kuwezesha yote ambayo ni muhimu kwa ajili ya wokovu.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page