Msukumo Hatarishi
- Dalvin Mwamakula
- Apr 28
- 2 min read
Updated: May 1

“Au ni nani aliyempa chochote [Mungu] ili arudishiwe?” Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, viko kwake, na kwa ajili yake. Utukufu uwe kwake yeye milele. (Warumi 11:35-36)
Kwenye suala la utii, shukrani ni msukumo hatarishi. Inaelekea kuonyeshwa kwa masharti ya mdaiwa. Kwa mfano, “Angalia kiasi gani Mungu amefanya kwa ajili yako. Je, haikupasi wewe kufanya mengi kwa ajili yake kwa sababu ya shukrani?” Au, “Una deni kwa Mungu kwa kila namna ulivyo na kila ulichonacho. Je, umefanya nini kwa ajili yake kama hisani ya kurudisha fadhila kwa malipo?”
Nina shida angalau tatu na aina hii ya msukumo.
Imani inatazama ahadi, nitakuwa "pamoja nawe popote uendako", na kisha hujitokeza, kwa utii, kuichukua nchi.
Kwanza, haiwezekani kumlipa Mungu kwa neema zote alizotupa. Hatuwezi hata kuanza kumlipa, kwa sababu Warumi 11:35–36 inasema, “'Ni nani aliyempa [Mungu] chochote ili alipwe?' [Jibu: Hakuna!] Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake na kwa njia yake na kwake yeye. Utukufu uwe kwake yeye milele.” Hatuwezi kumlipa kwa sababu yeye tayari ana miliki kila kitu tunachopaswa kumpa - ikiwa ni pamoja na jitihada zetu zote.
Pili, hata kama tungelifaulu kumlipa kwa neema yake yote kwetu, tungelifaulu tu kugeuza neema kuwa shughuli ya biashara ya mabadilishano. Ikiwa tunaweza kumlipa, haikuwa neema Ikiwa mtu anajaribu kukuonyesha upendeleo maalum wa upendo kwa kukukaribisha kwenye chakula cha jioni, kisha unamaliza jioni kwa kusema kwamba utamlipa kwa kuwaalika kwako wiki ijayo, unabatilisha neema yao na kuifanya kuwa biashara. Mungu hapendi neema yake ibatilishwe. Anapenda kwamba ipate kutukuzwa (Waefeso 1:6,12,14).
Tatu, kuzingatia shukrani kama nia ya utii huelekea kupuuzia umuhimu wa dhati wa kuwa na imani katika neema ya Mungu ya wakati ujao. Shukrani hutazama nyuma kwa neema iliyopokelewa siku za nyuma na huhisi shukrani. Imani inatazamia neema iliyoahidiwa katika siku zijazo - iwe dakika tano kutoka sasa au karne tano kutoka sasa - na inahisi kuwa na matumaini. “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo” (Waebrania 11:1).
Imani hii katika neema ya wakati ujao ndiyo msukumo wa utii unaohifadhi ubora wa neema wa utii wa mwanadamu. Utii haujumuishi katika kumlipa Mungu na hivyo kugeuza neema kuwa biashara. Utii unatokana na kumwamini Mungu kwa neema zaidi - neema ya wakati ujao - na hivyo kutukuza rasilimali zisizo na mwisho za upendo na nguvu za Mungu. Imani inatazama ahadi, nitakuwa "pamoja nawe popote uendako" (Yoshua 1:9), na kisha hujitokeza, kwa utii, kuichukua nchi.




Comments