Mtazame Yesu kwa ajili ya Furaha Yako
- Dalvin Mwamakula
- Feb 26
- 2 min read

"Wanafanya matendo yao yote ili waonekane na wengine. . . . Wanapenda nafasi za heshima kwenye karamu na viti bora katika masinagogi, na salamu sokoni na kuitwa rabi na wengine." (Mathayo 23:5–7)
Mwasho wa kujipenda unatafuta mkuno wa kujiridhisha. Ikiwa tunapata furaha yetu kutokana na kujihisi tunajitosheleza, hatutaridhika bila wengine kuona na kushangilia kujitosheleza kwetu.
Hivyo ndivyo Yesu alivyoelezea waandishi na Mafarisayo katika Mathayo 23:5, “Wanafanya matendo yao yote ili waonekane na wengine.”
Hii ipo kinyume na matarajio. Je, huoni kwamba kujitosheleza kunapaswa kumwondolea mtu mwenye kiburi haja ya kusifiwa na wengine? Hivyo ndivyo “kujitosheleza” kunavyomaanisha. Lakini ni wazi kuna upungufu, utupu katika hali hii inayoitwa kujitosheleza.
Nafsi haikuundwa kujitosheleza au kujitegemea yenyewe. Haiwezi kamwe kujitosheleza yenyewe. Sisi sio Mungu. Tupo katika mfano wa Mungu. Na kinachotufanya kuwa “kama” Mungu si kujitosheleza kwetu. Sisi ni vivuli na sauti za mwangwi. Kwa hivyo, daima kutakuwa na utupu katika roho unaojitahidi kuridhika na rasilimali binafsi.
Mwasho wa kujipenda hutafuta kujiridhisha, lakini nafsi haikuundwa kujitosheleza— ukamilifu hupatikana katika kuridhika na jinsi Mungu alivyo kwetu ndani ya Yesu.
Hamu hii tupu ya kusifiwa na wengine inaashiria kushindwa kwa kiburi na ukosefu wa imani katika neema inayoendelea ya Mungu. Yesu aliona athari mbaya ya tamaa hii ya utukufu wa kibinadamu. Aliitaja katika Yohana 5:44, “Mnawezaje kuamini, mnapopokea utukufu kutoka kwa kila mmoja wenu na hamtafuti utukufu unaotoka kwa Mungu pekee?” Jibu ni kwamba, huwezi. Kutamani sifa kutoka kwa watu wengine hufanya imani kuwa haiwezekani. Kwanini?
Kwa sababu imani huacha kujiangalia binafsi na kumuelekea Mungu. Imani ni kuridhika na yote ambayo Mungu ni kwa ajili yako katika Yesu. Na ikiwa unatafuta kuridhika kwa tamaa yako kutoka kwa sifa za wengine, utageuka mbali na Yesu. Yeye hayupo hivyo. Anaishi kwa ajili ya utukufu wa Baba yake. Na anatuita tufanye vivyo hivyo.
Lakini ikiwa utageuka kutoka kujiridhisha mwenyewe (toba), na kumjia Yesu kwa ajili ya kufurahia yote ambayo Mungu yuko kwetu ndani yake (imani), basi tamaa ya utupu itabadilishwa na ukamilifu — kile ambacho Yesu anaita “chemchemi ya maji inayobubujika hadi uzima wa milele” (Yohana 4:14).




Comments