Mtukuze Mungu kwa Kushukuru
- Dalvin Mwamakula
- Nov 14
- 2 min read

Haya yote ni kwa ajili yenu, ili kwamba kadiri neema inavyoenea kwa watu wengi zaidi na zaidi izidi kutoa shukrani kwa utukufu wa Mungu. (2 Wakorintho 4:15)
Shukrani kwa Mungu ni hisia ya furaha. Tuna hisia ya deni la furaha kwa neema yake. Kwa hivyo kwa namna fulani katika hisia ya shukrani, sisi bado ni wanufaikaji. Lakini kwa asili yake, shukrani humtukuza mtoaji. Tunapohisi shukrani, tunakubali hitaji letu na wema wa Mungu, utimilifu wa Mungu, utajiri wa utukufu wake.
Kama vile ninavyojinyenyekeza na kumwinua mhudumu katika mgahawa ninaposema, “Asante,” kwa hivyo mimi hujinyenyekeza na kumuinua Mungu ninapohisi shukrani kwake. Tofauti, bila shaka, ni kwamba kwa kweli nina deni kubwa kwa Mungu kwa ajili ya neema yake, na kila kitu anachonifanyia ni bure na sistahili.
Lakini hoja ni kwamba shukrani humtukuza mtoaji. Inamtukuza Mungu. Na hili ndilo lengo la mwisho la Paulo katika kazi zake zote. Ndiyo, kazi yake ni kwa ajili ya kanisa - mema ya kanisa. Lakini kanisa sio lengo la juu zaidi. Sikiliza tena: “Yote ni kwa ajili yenu, ili kwamba kadiri neema inavyoenea kwa watu wengi zaidi na zaidi na zaidi shukrani, kwa utukufu wa Mungu. Yote kwa ajili yenu - kwa ajili ya utukufu wa Mungu!
Jambo la ajabu kuhusu injili ni kwamba mwitikio unaohitaji kutoka kwetu kwa ajili ya utukufu wa Mungu pia ni mwitikio ambalo ni wa kawaida na wa furaha; yaani, shukrani kwa ajili ya neema. Utukufu wa Mungu katika kutoa na furaha yetu ya unyenyekevu katika kupokea hazipo katika mashindano. Shukrani zenye furuha humtukuza Mungu.
Maisha yanayomtukuza Mungu kwa neema yake na maisha ya furaha kuu ni maisha yale yale. Na kinachoyafanya yawe kitu kimoja ni kushukuru.




Comments