Mtumikie Mungu kwa Kiu yako
- Dalvin Mwamakula
- May 29
- 2 min read

Kwa hiyo, kama tuko katika mwili huu au tuko mbali nao, lengo letu ni kumpendeza Bwana. (2 Wakorintho 5:9)
Je, utafanyaje ukigundua (kama Mafarisayo walivyofanya) kwamba ulikuwa umejitolea maisha yako yote kujaribu kumpendeza Mungu, lakini muda wote ulikuwa ukifanya mambo ambayo machoni pa Mungu yalikuwa machukizo (Luka 16:14–15)?
Mtu anaweza kuhoji hili na kusema, “Sidhani hilo linawezekana; Mungu hatamkataa mtu ambaye amekuwa akijaribu kumpendeza.” Lakini unaona huyu muulizaji amefanya nini? Ameweka ushawishi wake juu ya kile ambacho kingempendeza Mungu juu ya wazo lake la jinsi Mungu alivyo. Hiyo ndiyo sababu hasa ni lazima tuanze na tabia ya Mungu iliyofunuliwa katika Maandiko.
Mungu ni chemchemi ya mlima, sio chombo cha umwagiliaji. Chemchemi ya mlima inajijaza yenyewe. Inafurika kila wakati na kuwapa wengine. Lakini chombo cha umwagiliaji kinahitaji kujazwa na pampu au ndoo.
Kwa hiyo, swali kuu ni:
Je, unaihudumiaje chemchemi? Je, unahudumiaje chombo cha umwagiliaji? Je, unamtukuzaje Mungu kwa jinsi alivyo halisi?
Ikiwa unataka kutukuza thamani ya chombo cha kumwagilia, unafanya kazi kwa bidii ili kiwe kimejaa na kitumike kwa manufaa. Lakini ukitaka kutukuza thamani ya chemchemi, fanya hivyo kwa kupiga magoti na mikono yako na kunywa kwa kuuridhisha moyo wako, mpaka upate kiburudisho na nguvu za kurudi bondeni na kuwaambia watu kile ulichokipata.
Tumaini langu kama mwenye dhambi aliyekata tamaa hutegemea ukweli huu wa Biblia: kwamba Mungu ni aina ya Mungu ambaye atapendezwa na jambo moja ninalopaswa kutoa: kiu yangu. Ndio maana uhuru wa enzi kuu na utoshelevu wa Mungu ni wa thamani sana kwangu: hivi ni msingi wa tumaini langu kwamba Mungu hafurahii ustadi wa majeshi za ndoo za umwagiliaji, lakini kwa kuinama kwa wenye dhambi waliovunjika kunywa kwenye chemchemi ya neema.
Kwa vyovyote vile tunapaswa kutafuta kumpendeza Mungu, sasa na hata milele. Lakini ole wetu ikiwa maisha yetu yote yamejengeka katika msingi wa maoni yasiyo ya kweli ya kile kinachompendeza Mungu. Bwana hafurahishwi na wale wanaomchukulia kama chombo cha umwagiliaji kwa uhitaji, bali kama chemchemi isiyokwisha na yenye kuridhisha. Kama vile Zaburi 147:11 inavyosema, “BWANA hupendezwa . . . katika wale wanaotumainia fadhili zake.




Comments