top of page

Mtumishi Mkuu

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Oct 7
  • 2 min read
ree

. . . ili katika nyakati zijazo aonyeshe wingi wa neema yake isiyopimika katika wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu. (Waefeso 2:7)

 

Kwangu mimi, taswira ya Biblia ya kustaajabisha zaidi ya ujio wa pili wa Kristo iko katika Luka 12:35–37 , ambayo inawakilisha kurudi kwa Bwana kutoka katika karamu ya ndoa kama hii:

 

“Kaeni mmevaa kwa ajili ya kazi na taa zenu zikiwaka, na iweni kama watu wanaomngojea bwana wao arudi kutoka harusini, ili wamfungulie mlango mara ajapo na kubisha hodi. Heri watumishi wale ambao Bwana wao atawakuta wamekesha ajapo. Kweli, nawaambia, atajivika mavazi ya utumishi na kuwaweka mezani, kisha atakuja na kuwahudumia."

 

Ili kuwa na uhakika, tunaitwa watumishi - na hiyo bila shaka ina maana kwamba tunapaswa kufanya vile tulivyoambiwa. Lakini maajabu ya picha hii ni kwamba "bwana" anasisitiza kuhusu kutumikia . Huenda tulitarajia hili wakati wa huduma ya Yesu duniani, kwa kuwa alisema, “Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi” (Marko 10:45). Lakini Luka 12:35–37 ni picha ya ujio wa pili, wakati Mwana wa Adamu ajapo katika utukufu unaopofusha wa Baba yake “pamoja na malaika zake wenye nguvu katika mwali wa moto” kama 2 Wathesalonike 1:7–8 inavyosema. Kwanini Yesu angeonyeshwa kama mhudumu wa meza katika kuja kwake kwa pili?

 

Kwasababu kiini cha utukufu wake ni utimilifu wa neema inayofurika katika wema kwa wahitaji.

Hii ndiyo sababu Waefeso 2:7 inasema analenga “katika nyakati zijazo [kuonyesha] wingi wa neema yake isiyopimika katika wema kwetu sisi katika Kristo Yesu.”

 

Ukuu wa Mungu wetu ni nini? Upekee wake ni upi duniani? Isaya anajibu hivi:


“Tangu zamani hakuna aliyesikia, wala hakutambua kwa sikio, wala hakuna jicho lililomwona Mungu ila wewe, awatendaye kazi wamngojao” (Isaya 64:4).


Hakuna mungu mwingine kama huyu. Yeye haachi kamwe jukumu la mfadhili asiye na ukomoo wa watu wake wanaomtegemea daima, wenye furaha.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page