top of page

Mtumishi wetu, Yesu

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Jan 27
  • 2 min read
ree

“Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.” (Marko 10:45)


Sio tu kwamba alikuwa mtumishi wa watu wake alipokuwa akiishi duniani, lakini pia atakuwa mtumishi wetu atakapokuja tena. “Amin, nawaambia, atajivika utumishi, na kuwaketisha mezani, naye atakuja na kuwahudumia” (Luka 12:37). Yesu alitoa hiyo kama picha ya kile atakachofanya wakati wa kurudi kwake.


Si hivyo tu, yeye ni mtumishi wetu sasa. “'Sitakuacha kamwe wala sitakutupa.' Kwa hiyo tunaweza kusema kwa ujasiri, ‘Bwana ndiye msaidizi wangu; sitaogopa; mwanadamu atanitenda nini?’” (Waebrania 13:5–6).


Je, hii inamdharau Kristo aliyefufuka — kusema kwamba alikuwa, ni, na atakuwa mtumishi wa watu wake? Ingekuwa hivyo, ikiwa neno “mtumishi” lilimaanisha “mtu anayechukua amri,” au ikiwa tulifikiri sisi ni mabwana zake. Ndiyo, hilo lingemvunjia heshima. Lakini haimvunjii heshima kusema kwamba sisi ni dhaifu na tunahitaji msaada wake.


Haimvunjii heshima kusema kwamba yeye peke yake ndiye anayeweza kutuhudumia kwa kile tunachohitaji zaidi.

Haimvunjii heshima kusema kwamba yeye ni chemchemi isiyoisha ya upendo, na kwamba kadiri anavyotusaidia zaidi na kadiri tunavyotegemea utumishi wake, ndivyo rasilimali zake zinavyoonekana kuwa za kushangaza zaidi. Kwa hiyo, tunaweza kusema kwa uhakika, “Yesu Kristo yu hai kutumikia!”


Yuko hai kuokoa. Yuko hai kutoa. Na anafurahi kuwa hivi. 

Yeye si wa kuelemewa na wasiwasi wako. Yeye hustawi kwa kubeba mizigo, si kutwisha mizigo. Anapenda kufanya kazi "kwa ajili ya wale wanaomngojea" (Isaya 64: 4). Yeye “hufurahia . . . wale wanaotumainia fadhili zake” (Zaburi 147:11). Macho yake “hukimbiakimbia duniani kote ili kujionyesha mwenye nguvu kwa ajili ya wale ambao mioyo yao inamtegemea kwa ukamilifu” (2 Mambo ya Nyakati 16:9).


Yesu Kristo anachangamka kwa utumishi wenye uwezo wote kwa ajili ya wote wanaomtumaini.




Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page