Muhtasari wa Injili kwa hoja Sita
- Dalvin Mwamakula
- Feb 26
- 3 min read

Kristo pia aliteseka mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili ya wasio haki, ili atulete kwa Mungu. (1 Petro 3:18)
Huu hapa ni muhtasari wa injili ili kukusaidia kuielewa, kuifurahia, na kuishirikisha!
Mungu alituumba sisi kwa ajili ya utukufu wake.
"Walete wana wangu kutoka mbali na binti zangu kutoka miisho ya dunia, kila mmoja anayeitwa kwa jina langu, niliyemuumba kwa ajili ya utukufu wangu" (Isaya 43:6–7).
Mungu alituumba sote kwa mfano wake ili tuweze kuonyesha, au kuakisi, tabia yake na uzuri wa maadili yake.
Kwa hiyo kila mwanadamu anapaswa kuishi kwa ajili ya utukufu wa Mungu.
"Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu" (Wakorintho 10:31).
Njia ya kuishi kwa utukufu wa Mungu ni kumpenda (Mathayo 22:37),
kumtumaini (Warumi 4:20),
kumshukuru (Zaburi 50:23),
kumtii (Mathayo 5:16),
na kumthamini zaidi ya vitu vyote (Wafilipi 3:8; Mathayo 10:37).
Tunapofanya mambo haya tunaonyesha utukufu wa Mungu.
Hata hivyo, sote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.
"Wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu" (Warumi 3:23).
"Ingawa walimjua Mungu, hawa kumtukuza kama Mungu wala kumshukuru . . . waka ubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sanamu" (Warumi 1:21-23).
Hakuna mmoja wetu ambaye amempenda, kumtumaini, kumshukuru, kumtii, au kumthamini Mungu kama tunavyopaswa.
Kwa hiyo sote tunastahili adhabu ya milele.
"Mshahara wa dhambi ni mauti ya milele, lakini zawadi ya bure ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu." (Warumi 6:23).
Wale ambao hawa kumtii Bwana Yesu "wataadhibiwa kwa maangamizi ya milele, mbali na uwepo wa Bwana na utukufu wa nguvu zake" (2 Wathesalonike 1:9).
"Hawa wataenda kwenye adhabu ya milele, lakini wenye haki wataingia kwenye uzima wa milele" (Mathayo 25:46).
5) Lakini, kwa huruma yake kuu, Mungu alimtuma Mwana wake wa pekee Yesu Kristo ulimwenguni ili kuwapatia wenye dhambi njia ya uzima wa milele.
"Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu kiasi kwamba akamtoa Mwana wake wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele" (Yohana 3:16).
"Kristo alitukomboa kutoka laana ya sheria kwa kufanyika laana kwa ajili yetu"
"Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu" (1 Petro 3:18).
6) Kwa hiyo, uzima wa milele ni zawadi ya bure kwa wote watakao mwamini Kristo kama Bwana na Mwokozi na Hazina kuu ya maisha yao.
"Amini katika Bwana Yesu, nawe utaokoka" (Matendo ya Mitume 16:31).
"Ukiungama kwa kinywa chako kwamba Yesu ni Bwana na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka" (Warumi 10:9).
"Kwa neema mmeokolewa kwa njia ya imani. Na hii sio kazi yako mwenyewe; ni zawadi cha Mungu, wala si matokeo ya matendo, mtu awaye yote asije akajisifu” (Waefeso 2:8–9).
"Nimesulubiwa pamoja na Kristo. Si mimi tena ninayeishi, bali Kristo anaishi ndani yangu. Na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu" (Wagalatia 2:20).
"Nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu Kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote na kuyahesabu kuwa kama mavi, ili nipate Kristo" (Wafilipi 3:8).
Comments