Mungu Anafanya Kazi Kwa Ajili Yako
- Dalvin Mwamakula
- Apr 28
- 2 min read
Updated: May 1

Ninainua macho yangu niitazame milima. Msaada wangu unatoka wapi? Msaada wangu u katika Bwana, aliyezifanya mbingu na nchi. Hatauacha mguu wako usogezwe; hatasinzia yeye akulindaye. (Zaburi 121:1-3)
Je, unahitaji msaada? Mimi Nahitaji. Unatafuta wapi msaada?
Wakati mtunga zaburi alipoinua macho yake kuelekea milima na kuuliza, “Msaada wangu utatoka wapi?” akajibu, “Msaada wangu unatoka kwa Bwana,” sio kutoka milima, bali kwa Mungu aliyeumba milima.
"Msaada wangu u katika Bwana, aliyeumba mbingu na nchi ."
Kwa hiyo, alijikumbusha kweli mbili kuu: Moja ni kwamba Mungu ni Muumba mwenye uwezo juu ya matatizo yote ya maisha; nyingine ni kwamba Mungu hasinzii kamwe. "Yeye akulindaye hatasinzia."
Mungu ni mtenda kazi asiyechoka. Yeye hachoki kamwe. Mfikirie Mungu kama mfanyakazi katika maisha yako. Ndiyo, hili ni la ajabu. Tuna mwelekeo wa kujifikiria kama wafanyikazi katika maisha ya Mungu. Lakini Biblia inatutaka kwanza tustaajabie kwamba Mungu ni mtenda kazi katika maisha yetu: “Tangu zama za kale hakuna aliyesikia, wala kutambua kwa sikio, wala hakuna jicho lililomwona Mungu zaidi yako wewe, atendaye kazi kwa ajili ya hao wamngojao ” (Isaya 64:4).
Mungu anatufanyia kazi masaa yote. Hachukui siku za mapumziko na wala halali. Kwa kweli ana shauku sana ya kufanya kazi kwa ajili yetu hivi kwamba anazunguka kutafuta kazi zaidi ya kufanya kwa ajili ya watu wanaomtumaini: “Macho ya Bwana hukimbia kimbia duniani kote, ili kuwapa msaada mkubwa wale mioyo ya mwao haina hatia kwake” (2 Mambo ya Nyakati 16:9).
Mungu anapenda kuonyesha nguvu zake bila kuchoka na hekima na wema wake kwa kuwafanyia kazi watu wanaomtumaini. Kutumwa kwa Mwanawe, Yesu, ilikuwa njia kuu ambayo Baba alionyesha hii: "Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa bali kutumika" (Marko 10:45). Yesu anafanya kazi kwa ajili ya wafuasi wake. Anawahudumia. Injili sio bango lisemalo "msaada unaohitajika". Ni bango lisemalo "msaada unapatikana".
Hili ndilo tunalopaswa kuamini - kuamini kweli - ili "kufurahi siku zote" (1 Wathesalonike 5:16) na "kushukuru siku zote na kwa kila kitu" (Waefeso 5: 20) na tunayo "amani ya Mungu, ambayo yapita fahamu zote” (Wafilipi 4:7), na “msijisumbukie lo lote” (Wafilipi 4:6), na kuchukia maisha yetu “katika ulimwengu huu” (Yohana 12:25), na “kumpenda jirani [yetu] kama [sisi wenyewe]” (Mathayo 22:39).
Ukweli ulioje! Ni uhalisia ulioje! Mungu yuko macho usiku kucha na mchana kutwa kufanya kazi kwa ajili ya wale wanaomngoja.
Comments