top of page

Mungu Anapoapa kwa Mungu

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Nov 14
  • 1 min read
ree

Aliapa kwa jina lake mwe nyewe kwa kuwa hapakuwa na mkuu kuliko yeye ambaye angeweza kuapa kwa jina lake. Alisema, “Hakika nitakubariki na kukupatia watoto wengi.” (Waebrania 6:13-14)


Kuna Mtu mmoja ambaye thamani yake na heshima na adhama na thamani na ukuu na uzuri na sifa ni zaidi ya maadili mengine yote pamoja - mara elfu kumi zaidi - yaani, Mungu mwenyewe. Kwa hiyo, Mungu anapoapa, anaapa kwa nafsi yake mweyewe. 


Ikiwa angeweza kwenda juu zaidi, angeenda juu zaidi. Kwanini? Ili kukutia moyo wa nguvu katika tumaini lako.


Mungu anachosema katika kuapa kwa nafsi yake ni kwamba haiwezekani kabisa kwake kuvunja neno lake la ahadi ya kutubariki kama isivyowezekana kwake kujidharau mwenyewe. 

Mungu ndiye thamani kuu katika ulimwengu. Hakuna kitu cha thamani zaidi au cha ajabu kuliko Mungu. Kwa hiyo, Mungu anaapa kwa Mungu. Na kwa kufanya hivyo anasema, “Namaanisha wewe uwe na imani nyingi ndani yangu kadiri inavyowezekana kuwa nayo.” Kwa maana kama ingewezekana zaidi, Waebrania 6:13 inasema, angalitupa hivyo. “Kwa kuwa hakuwa na mkubwa zaidi wa kuapa kwake, aliapa kwa nafsi yake. 


Sasa huyu ndiye Mungu wetu, Mungu anayefikia juu awezavyo ili kutia tumaini lenu lisilotikisika ndani yake. Kwa hiyo, mkimbilie Mungu kwa ajili ya kimbilio. Geuka kutoka kwenye matumaini yote ya juu juu, yenye kujishinda ya ulimwengu, na uweke tumaini lako kwa Mungu. Hakuna kitu na hakuna kama Mungu aliye kimbilio na mwamba wa tumaini.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page