Mungu Atakutimizia Mahitaji Yako Yote
- Dalvin Mwamakula
- Sep 2
- 1 min read

Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu (Wafilipi 4:19).
Katika Wafilipi 4:6 , Paulo anasema, “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.” Na kisha katika Wafilipi 4:19 (mistari 13 tu baadaye), anatoa ahadi ya ukombozi ya neema ya wakati ujao: “Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.”
Ikiwa tutaishi kwa imani katika ahadi hii ya neema ya wakati ujao, itakuwa vigumu sana kwa wasiwasi kuishi ndani yetu. “Utajiri katika utukufu” wa Mungu hauwezi kuisha. Kwa kweli anamaanisha kwamba tusiwe na wasiwasi kuhusu wakati wetu ujao.
Tunapaswa kufuata utaratibu huu ambao Paulo anaweka kwa ajili yetu.
Tunapaswa kupigana na kutokuamini kwa wasiwasi kwa kutumia ahadi za neema ya wakati ujao.
Wakati ninapokuwa na wasiwasi kuhusu jambo jipya lenye hatari au mkutano, mara kwa mara napambana na kutoamini kwa kutumia moja ya ahadi zangu zinazotumika sana, Isaya 41:10 .
Siku nilipoondoka Marekani kwa miaka mitatu kwenda Ujerumani baba yangu alinipigia simu kwa umbali mrefu na kunipa ahadi hii kwenye simu. Kwa miaka mitatu lazima niliinukuu mara mia tano ili kunipitisha katika vipindi vya mfadhaiko mkubwa. “Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; Nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.”
Nimepambana na wasiwasi kwa ahadi hii mara nyingi sana kiasi kwamba wakati mota ya akili yangu ipo gia ya 'free', mlio wa gia ni sauti ya Isaya 41:10.




Comments