Mungu Hufanya Kazi Kupitia Maazimio Mema
- Dalvin Mwamakula
- Feb 26
- 2 min read

Kwa ajili hiyo twawaombea ninyi daima, ili Mungu wetu awafanye ninyi kustahili wito wake na kutimiza kila kusudi la wema na kila kazi ya imani kwa nguvu zake. (2 Wathesalonike 1:11)
Kutafuta nguvu za Mungu ili kutimiza maazimio yetu mema haimaanishi kwamba hatuazimii kweli, au kwamba hatutumii nguvu ya nia.
Kutegemea nguvu za Mungu hakuchukui nafasi ya kutumia maamuzi yetu! Nguvu za Mungu katika utakaso hazitufanyi kuwa wanyonge-tegemezi! Nguvu za Mungu zinajihusisha chini au nyuma na ndani ya mapenzi yetu, si badala ya mapenzi yetu.
Ushahidi wa nguvu za Mungu katika maisha yetu siyo ukosefu wa mapenzi yetu, bali ni nguvu ya mapenzi yetu, furaha ya mapenzi yetu.
Yeyote anayesema, “Naam, naamini katika ukuu wa Mungu kwa hiyo nitakaa tu na sitofanya chochote” haamini kweli katika ukuu wa Mungu. Kwa nini mtu anayemwamini Mungu katika enzi ya ukuu wake aonyeshe kutokutii waziwazi?
Mungu hataonekana kwa nguvu katika nia yako kwa njia nyingine yoyote isipokuwa kupitia matumizi yako ya nia— kupitia maazimio yako mazuri, mipango, na makusudi yako.
Unapokaa bila kufanya chochote, si kwamba wewe haufanyi chochote. Unatumia hiari yako kwa makusudi kuamua kukaa bila kufanya chochote. Na ikiwa hivyo ndivyo unavyoshughulikia dhambi au majaribu katika maisha yako, ni uasi wa wazi, kwa sababu tumeamriwa kupigana vita vizuri (1 Timotheo 1:18) na kumpinga shetani (Yakobo 4:7) na kujitahidi kuwa watakatifu (Waebrania 12:14) na kuyaua matendo ya dhambi ya mwili (Warumi 8:13).
2 Wathesalonike 1:11 inasema kwamba ni kwa nguvu za Mungu tutatimiza nia zetu nzuri na kazi zetu za imani. Lakini hii haifuti maana ya neno “nia” na neno “kazi.” Sehemu ya mchakato mzima wa kutembea kwa kustahili mwito wa Mungu ni kushiriki kikamilifu nia yetu katika kuamua kutenda haki.
Kama una dhambi inayokaa katika maisha yako, au kama unaendelea kupuuza tendo jema kwa sababu tu umekuwa ukisubiri kuokolewa bila kupambana, unazidisha kutotii kwako. Mungu kamwe hataonekana kwa nguvu katika nia yako kwa njia nyingine yoyote isipokuwa kupitia matumizi yako ya nia hiyo; yaani, kupitia maazimio yako mazuri — nia zako nzuri, mipango na makusudi yako.
Kwa hiyo, watu wanaoamini katika ukuu wa Mungu hawapaswi kuogopa kushiriki nia zao katika mapambano ya utakatifu. "Jitahidini kuingia kwa kupitia mlango mwembamba. Maana nawaambia, wengi watajaribu kuingia lakini hawataweza." (Luka 13:24). Jitahidini tu katika imani kwamba katika na kupitia jitihada zenu Mungu anafanya kazi ili kutaka na kutenda kulingana na mapenzi yake mema (Wafilipi 2:13).
コメント