top of page

Mungu Huponya kwa Kunyenyekeza

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Oct 7
  • 2 min read
ree

“Nimeziona njia zake, lakini nitamponya; Nitamwongoza na kumrudishia faraja yeye na waombolezaji wake, nikiumba matunda ya midomo. Amani, amani, kwao walio mbali na walio karibu, asema Bwana, nami nitamponya. (Isaya 57:18-19)

 

Licha ya ukali wa ugonjwa wa uasi na ukaidi wa mwanadamu, Mungu ataponya. Je, ataponya vipi? Isaya 57:15 inasema kwamba Mungu anakaa pamoja na waliopondwa na wanyenyekevu. Lakini watu wa Isaya 57:17 si wanyenyekevu. Wanafuata njia yao ya kiburi bila aibu. Kwahiyo, uponyaji utakuwa nini?

 

Inaweza kuwa kitu kimoja tu.


Mungu atawaponya kwa kuwanyenyekeza. Atamponya mgonjwa kwa kukiponda kiburi chake.

Ikiwa tu waliopondwa na wanyenyekevu watafurahia ushirika wa Mungu (Isaya 57:15), na ikiwa ugonjwa wa Israeli ni uasi wa kiburi na wa makusudi (Isaya 57:17), na ikiwa Mungu anaahidi kuwaponya (Isaya 57:18), basi uponyaji wake lazima uwe kunyenyekea na tiba yake lazima iwe roho iliyopondeka.

 

Je, hii si njia ya Isaya ya kutabiri kile Yeremia alichokiita agano jipya na zawadi ya moyo mpya? Akasema, tazama, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli. . . . Nitaweka sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika. Nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu” (Yeremia 31:31 , 33).

 

Isaya na Yeremia wote wanaona wakati ujao ambapo watu wagonjwa, wasiotii, na wenye mioyo migumu watabadilishwa kwa njia ya kimiujiza. Isaya anazungumza juu ya uponyaji. Yeremia anazungumza juu ya kuandika sheria kwenye mioyo yao. Naye Ezekieli anaiweka hivi: “Nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu. Nami nitauondoa moyo wa jiwe katika mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama” (Ezekieli 36:26

 

Kwa hiyo uponyaji wa Isaya 57:18 ni upandikizaji mkubwa wa moyo — ule moyo wa zamani uliokuwa mgumu, wenye kiburi, na wenye ukaidi una ondolewa, na moyo mpya laini na mpole unawekwa ambao unanyenyekezwa kwa urahisi na kupondwa na kumbukumbu ya dhambi na dhambi iliyobaki. 

 

Huu ni moyo ambao Aliyetukuka ambaye jina lake ni Mtakatifu atakaa nao milele.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page