top of page

Mungu Hututia Nguvu Kupitia Wengine

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Mar 31
  • 1 min read

Updated: Apr 4

“Simoni, Simoni, sikiliza, Shetani ameomba kuwapepeta ninyi wote kama ngano, lakini nimekuombea wewe Simoni ili imani yako isishindwe. Nawe ukiisha kunirudia, uwaimarishe ndugu zako.” (Luka 22:31-32)


Vipi kuhusu wale mitume wengine kumi (bila kuhesabu Yuda)?


Shetani alikuwa anataka kuwachambua pia. Je, Yesu aliwaombea?


Ndiyo aliwaombea. Lakini hakumwomba Baba alinde imani yao kwa njia ile ile alivyoilinda ya Petro.

Mungu alivunja kiburi na kujitegemea kwa Petro usiku ule katika uchungu wa kuchambuliwa na Shetani. Lakini hakumwacha aende zake. Alimgeuza na kumsamehe na kumrejesha na kuimarisha imani yake. Na sasa ilikuwa kazi ya Petro kuwatia nguvu wale wengine kumi. "Na utakapogeuka, waimarishe ndugu zako."


Yesu aliwatunza wale kumi kwa kumtunza Petro. Aliyeimarishwa anakuwa mwenye kuimarisha.

Kuna somo kubwa hapa kwa ajili yetu. Wakati mwingine Mungu atakushughulikia moja kwa moja, akikuimarisha imani yako peke yako katika saa za alfajiri wakati kila mtu mwingine amelala. Lakini mara nyingi (tunaweza kusema mara kumi na moja kati ya kumi na mbili) Mungu huimarisha imani yetu kupitia mtu mwingine.


Mungu hututumia kina Simoni Petro ambao huleta neno la neema tunalohitaji ili kuendelea katika imani: kama ushuhuda kuhusu jinsi “Kilio chaweza kukaa usiku kucha, lakini furaha huja asubuhi” (Zaburi 30:5).


Usalama wa milele ni mradi wa jamii. Kila wakati Mungu anapouhimiza moyo wako kwa kutumia ahadi kwamba katika majaribio makali ya Shetani imani yako haitashindwa, chukua himizo hilo na uongeze furaha yako kwa kulitumia kuimarisha ndugu na jamaa zako — kwa nguvu zile zile ulizoimarishwa nazo.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page