top of page

Mungu Mwenye Furaha

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Sep 30
  • 2 min read
ree

Mafundisho ya kweli ambayo yanakubaliana na Injili ya utukufu wa Mungu anayehimidiwa [yaani, mwenye furaha]. (1 Timotheo 1:10-11)


Sehemu kubwa ya utukufu wa Mungu ni furaha yake.

 

Iili kuwa isiyofikirika kwa mtume Paulo kwamba Mungu angeweza kunyimwa furaha isiyo na ukomo na bado awe mtukufu. Kuwa na utukufu usio na ukomo ilikuwa ni kuwa na furaha isiyo na ukomo. Alitumia maneno, “ utukufu wa Mungu mwenye furaha,” kwa sababu ni jambo tukufu kwa Mungu kuwa na furaha kama alivyo—furaha isiyo na kikomo.

 

Utukufu wa Mungu unajumuisha mengi katika ukweli kwamba yeye ni mwenye furaha kupita mawazo yetu yote.


Hii ndiyo injili: “Injili ya utukufu wa Mungu mwenye furaha.” Hiyo ni nukuu kutoka katika Biblia! Ni habari njema kwamba Mungu ana furaha ya utukufu.

 

Hakuna mtu ambaye angependa kukaa milele na Mungu asiye na furaha.


Ikiwa Mungu hana furaha, basi lengo la injili si lengo la furaha, na hiyo inamaanisha kuwa isingekuwa injili hata kidogo.

 

Lakini, kwa kweli, Yesu anatualika kukaa milele na Mungu mwenye furaha anaposema, "Ingia katika furaha ya bwana wako" (Mathayo 25:23). Yesu aliishi na kufa ili furaha yake - furaha ya Mungu - iwe ndani yetu na furaha yetu iwe kamili (Yohana 15:11;17:13). Kwa hiyo, injili ni “injili ya utukufu wa Mungu mwenye furaha.”

 

Furaha ya Mungu kwanza kabisa ni furaha ndani ya Mwana wake. Hivyo tunaposhiriki furaha ya Mungu, tunashiriki furaha ileile ambayo Baba anayo ndani ya Mwana.

 

Hii ndiyo sababu Yesu alimtambulisha Baba kwetu. Mwishoni mwa sala yake kuu katika Yohana 17, alimwambia Baba yake, “Nimewajulisha jina lako, na nitaendelea kuwajulisha hilo, ili pendo ulilonipenda mimi liwe ndani yao, na mimi ndani yao” (Yohana 17:26). Alimtambulisha Mungu ili furaha ya Mungu katika Mwana wake iwe ndani yetu na kuwa furaha yetu ndani yake.

 

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page