top of page

Mwisho wa Yote

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Apr 28
  • 2 min read

Updated: May 1

Kwa upendo alitangulia kutuchagua ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, kulingana na kusudi la mapenzi yake. (Waefeso 1:4-5)


Uzoefu wa Charles Spurgeon hauko nje ya uwezo wa Mkristo yeyote wa kawaida.

 

Spurgeon, aliyeishi kutoka 1834 hadi 1892, alikuwa wa mfanyakazi mwenza na rafiki wa George Mueller na Hudson Taylor. Alitumikia Metropolitan Tabernacle huko London kwa zaidi ya miaka thelathini kama mchungaji maarufu zaidi wa wakati wake.

 

Mahubiri yake yalikuwa na nguvu sana hivi kwamba watu waliongoka kwa Kristo kila juma. Mahubiri yake bado yanachapishwa leo na anashikiliwa na wengi kama mfano wa mvuna nafsi.

 

Anakumbuka tukio alipokuwa na umri wa miaka kumi na sita ambalo lilitengeneza maisha na huduma yake kwa siku zake zote.

 

Wakati nilipokuwa nakuja kwa Kristo, nilifikiri nilikuwa nikifanya yote mimi mwenyewe, na ingawa nilimtafuta Bwana kwa bidii, sikuwa na wazo kwamba Bwana alikuwa akinitafuta. Sidhani kwamba mwongofu mchanga analitambua hili mwanzoni.

 

Ninaweza kukumbuka siku na saa ile nilipopokea kwa mara ya kwanza kweli hizo [mafundisho ya neema kuu, neema ishindayo ] katika nafsi yangu—zilipochomwa moyoni mwangu kana kwamba kwa chuma cha moto, kama John Bunyan asemavyo. nakumbuka jinsi nilivyohisi kwamba nilikuwa nimekua, kwa ghafla, kutoka mtoto mchanga hadi kuwa mwanamume—kwamba nilikuwa nimefanya maendeleo katika ujuzi wa Maandiko, kwa kupata, mara moja kwa wote, dokezo hilo la kweli ya Mungu.

 

Usiku mmoja wa juma, nilipokuwa nimeketi katika nyumba ya Mungu, sikuwa nikifikiria sana mahubiri ya mhubiri, kwa maana sikuyaamini.

 

Wazo hilo lilinigusa, Je, ni kwa namna gani uliweza kuwa Mkristo? Nilimtafuta Bwana. Lakini ulikuwezaje kumtafuta Bwana? Ukweli uliangaza akilini mwangu kwa muda mfupi - sikupaswa kumtafuta isipokuwa kungekuwa na ushawishi fulani katika akili yangu wa kunifanya nimtafute. Niliomba, nilifikiri, lakini kisha nikajiuliza, Je, ni kwa namna gani nilifikia hitimisho la kuomba? Nilishawishiwa kufanya maombi kwa kusoma Maandiko. Ilikuwaje nikaanza kusoma Maandiko? Niliyasoma, lakini ni nini kilinifanya nifanye hivyo?

 

Kisha, kwa muda mfupi, nikaona kwamba Mungu alikuwa chanzo ya yote hayo , na kwamba alikuwa Mwanzilishi wa imani yangu, na hivyo mafundisho yote ya neema yalifunguliwa kwangu, na kutoka kwa fundisho hilo sijatoka hadi sasa, na ninatamani kufanya haya maungamo yangu ya mara kwa mara, “Naweka wazi mabadiliko yangu yametokana kabisa na Mungu.”

 

Vipi kuhusu wewe?


Je, unaweka wazi kuwa uongofu wako umetokana na Mungu kikamilifu? Je, yeye ndiye kiini cha yote? Je, hii inakufanya uusifu utukufu wa neema yake kuu, inayoshinda?

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page