top of page

Nafsi Yangu Ina Kiu ya Mungu

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Jul 31
  • 2 min read
ree

Kama vile ayala aoneavyo shauku vijito vya maji, ndivyo nafsi yangu ikuoneavyo shauku, Ee Mungu. Nafsi yangu inamwonea Mungu kiu, Mungu aliye hai. Ni lini nitaweza kwenda kukutana na Mungu? (Zaburi 42:1-2)

 

Kinachofanya jambo hili liwe zuri na muhimu sana kwetu ni kwamba hana kiu hasa ya kupata kitulizo kutokana na hali zake za kutisha. Yeye hana kiu hasa ya kutoroka kutoka kwa adui zake au uharibifu wao.

 

Si vibaya kutaka tulizo, na kuomba kwa ajili ya hilo. Wakati mwingine ni sawa kuomba kwa ajili ya kushindwa kwa maadui. Lakini muhimu zaidi kuliko hayo yote ni Mungu mwenyewe. 

 

Tunapofikiri na kuhisi pamoja na Mungu katika Zaburi, matokeo makuu ni haya:


Tunakuja kumpenda Mungu, na tunataka kumwona Mungu na kuwa na Mungu na kuridhika kwa kumtukuza na kumfurahia Mungu.

 

Tafsiri inayowezekana ya mwisho wa mstari wa 2 ni, “Ni lini nitakuja na kuuona uso wa Mungu?” Jibu la mwisho kwa swali hilo lilitolewa katika Yohana 14:9 na 2 Wakorintho 4:4. Yesu alisema, “Yeyote aliyeniona mimi amemwona Baba.” Na Paulo alisema kwamba tunapoongoka kwa Kristo tunaona “nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura ya Mungu.”

 

Tunapouona uso wa Kristo, tunauona uso wa Mungu. Na tunaona utukufu wa uso wa Kristo, Paulo anasema katika 2 Wakorintho 4:4 na 6 , tunaposikia hadithi ya injili ya kifo na ufufuo wake. Anaiita “injili ya utukufu wa Kristo, aliye sura ya Mungu.” Au (mstari wa 6): “maarifa ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.”

 

Bwana akuongezee njaa na kiu yako ya kuuona uso wa Mungu. Na akupe haja yako, hata leo, kupitia Injili ya utukufu wa Kristo, ambaye ni uso wa Mungu.

 

 

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page