Nani Alimuua Yesu?
- Dalvin Mwamakula
- May 29
- 2 min read

Ikiwa Mungu hakumhurumia Mwana-wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sote, atakosaje basi kutupatia vitu vyote kwa ukarimu pamoja naye ? (Warumi 8:32)
Mmoja wa marafiki zangu ambaye aliwahi kuwa mchungaji huko Illinois alikuwa akihubiri kwa kundi la wafungwa katika gereza la serikali kipidi cha Wiki Takatifu miaka kadhaa iliyopita. Katikati wa ujumbe wake, alisitisha na kuwauliza wanaume hao kama wanajua ni nani aliyemuua Yesu.
Wengine walisema maaskari walifanya hivyo. Wengine walisema Wayahudi walifanya hivyo. Wengine wakasema Pilato. Baadaye kulikuwapo na ukimya, rafiki yangu alisema kwa urahisi, "Baba yake ndiye aliyemuua."
Hivyo ndivyo nusu ya kwanza ya Warumi 8:32 inavyosema: Mungu hakumhurumia Mwanawe, bali alimtoa ili afe. “Huyu Yesu [alitolewa] kwa mpango ulio dhahiri na kujua kwake Mungu tangu zamani” (Matendo 2:23 . Isaya 53 inaiweka hata kwa uwazi zaidi, “Tulimdhania kuwa amepigwa, amepigwa na Mungu. . . . Yalikuwa mapenzi ya Bwana kumponda; yeye (Baba yake!) amemhuzunisha” (Isaya 53:4,10).
Au kama vile Warumi 3:25 inavyosema, “Mungu alimweka mbele awe upatanisho kwa damu yake.” Kama vile Ibrahimu alivyoinua kisu juu ya kifua cha mwanawe Isaka, lakini kisha akamhurumia mwanawe kwa sababu kulikuwa na kondoo katika kichaka, hivyo Mungu Baba aliinua kisu chake juu ya kifua cha Mwanawe, Yesu - lakini hakumhurumia, kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa kondoo; alikuwa mbadala.
Msingi wa ahadi ya neema ya Mungu ni kwamba Mwana wa Mungu alibeba adhabu yangu, ili niweze kusimama mbele ya Mungu nikiwa nimesamehewa na kufurahia ahadi za milele.
Mungu hakumhurumia Mwanawe, kwa sababu hiyo ndiyo ilikuwa njia pekee ambayo angeliweza kutuhurumia sisi na bado akabaki kuwa Mungu mwenye haki na mtakatifu. Hatia ya makosa yetu, adhabu ya maovu yetu, laana ya dhambi zetu ingelituleta bila kuepukika kwenye kuhangamia katika Jehanamu. Lakini Mungu hakumhurumia Mwanawe mwenyewe; alimtoa ili achomwe kwa ajili ya makosa yetu, na kupondwa kwa ajili ya maovu yetu, na kusulubiwa kwa ajili ya dhambi zetu.
Mstari huu— Warumi 8:32 —ndio mstari wa thamani zaidi katika Biblia kwangu kwa sababu msingi wa ahadi inayojumuisha yote ya neema ya Mungu ya wakati ujao ni kwamba Mwana wa Mungu alichukua katika mwili wake adhabu yangu yote na hatia yangu yote na hukumu yangu yote na lawama zangu zote na makosa yangu yote na upotovu wangu wote, ili niweze kusimama mbele ya Mungu mkuu na mtakatifu, kama aliyesamehewa, aliyepatanishwa, aliyehesabiwa haki, aliyekubaliwa, na mfaidika wa ahadi zisizosemeka za furaha milele na milele kwenye mkono wake wa kuume.




Comments