Neema kwa Kila Hitaji
- Dalvin Mwamakula
- Jun 30
- 1 min read

Nigeukie na unihurumie; mpe mtumishi wako nguvu zako. (Zaburi 86:16)
Neema ya wakati ujao ni ombi la kudumu la watunga zaburi wanaoomba. Wanasali tena na tena ili kukidhi kila hitaji. Wanatupa kielelezo kizuri cha utegemezi wa kila siku juu ya neema ya wakati ujao kwa kila jambo la lazima.
Wanalia kwa ajili ya neema wanapohitaji msaada: “Sikia, Ee Bwana, na unirehemu; Ee Bwana, uwe msaada wangu!” (Zaburi 30:10).
Wanapokuwa dhaifu: “Nigeukie na unihurumie; mpe mtumishi wako nguvu zako” (Zaburi 86:16).
Wanapohitaji uponyaji: “Unirehemu Bwana, kwa maana nimedhoofika; Ee Bwana, uniponye” (Zaburi 6:2).
Wanapoteswa na maadui: “Ee Bwana, tazama jinsi walivyo wengi adui zangu wanaonitesa!” (Zaburi 9:13).
Wanapokuwa wapweke: “Nigeukie na unihurumie, kwa maana ni mpweke na mwenye kuteseka” (Zaburi 25:16).
Wanapohuzunika: “Ee Bwana, unihurumie, kwa maana niko kwenye shida; macho yangu yanafifia kwa huzuni” (Zaburi 31:9).
Walipotenda dhambi: “Ee Bwana, nihurumie; niponye, kwa maana nimekutenda dhambi wewe!" (Zaburi 41:4).
Wanapotamani jina la Mungu litukuzwe kati ya mataifa: “Mungu aturehemu, na atubariki . . . ili njia zako zijulikane duniani” (Zaburi 67:1–2).
Bila shaka, maombi ni kiungo kikubwa cha imani kati ya nafsi ya mtakatifu na ahadi ya neema ya wakati ujao. Ikiwa huduma ilikusudiwa na Mungu kudumishwa kwa maombi, basi huduma ilikusudiwa kudumishwa na imani katika neema ya wakati ujao.




Comments