Neema ni Msamaha - na Nguvu!
- Dalvin Mwamakula
- May 29
- 2 min read

Kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo, na neema yake kwangu haikuwa bure. Badala yake, nilifanya kazi kwa bidii zaidi kuliko wengine wote, ingawa sio mimi, bali ni neema ya Mungu iliyo pamoja nami. (1 Wakorintho 15:10)
Neema sio tu upole wa Mungu tunapofanya dhambi.
Neema ni karama na uwezo kutoka kwa Mungu wa kutotenda dhambi. Neema ni nguvu, sio msamaha tu.
Hii ni wazi, kwa mfano, katika 1 Wakorintho 15:10. Paulo anaielezea neema kama nguvu iwezeshayo kazi yake. Sio tu msamaha wa dhambi zake; ni nguvu ya kuendelea katika utii. "Nalizidi kufanya kazi kuliko wengine wote, ingawa sio mimi, bali ni neema ya Mungu iliyo pamoja nami."
Kwa hiyo, jitihada tunazofanya ili kumtii Mungu sio jitihada zinazofanywa kwa nguvu zetu wenyewe, bali "kwa nguvu ambazo Mungu hutoa - ili Mungu atukuzwe katika kila kitu" (1 Petro 4:11). Ni utii wa imani. Imani katika uwezo wa neema ya Mungu unaokuja daima wa kutuwezesha kufanya yale tunayopaswa kufanya.
Paulo anathibitisha hili katika 2 Wathesalonike 1:11-12 kwa kuita kila moja ya matendo yetu ya wema kuwa "kazi ya imani," na kwa kusema kwamba utukufu huu huleta kwa Yesu "kulingana na neema ya Mungu wetu" kwa sababu hutokea " kwa uwezo wake.” Sikiliza misemo hiyo yote:
Kwa ajili hiyo twawaombea ninyi siku zote, ili Mungu wetu awafanye ninyi kustahili mwito wake, akamilishe kila nia ya wema na kila kazi ya imani kwa nguvu yake, ili jina la Bwana wetu Yesu litukuzwe ndani yenu, na ninyi ndani yake, kwa neema ya Mungu wetu na ya Bwana Yesu Kristo.
Utii unaomfurahisha Mungu unazalishwa na nguvu ya neema ya Mungu kwa njia ya imani. Nguvu hiyo hiyo inafanya kazi katika kila hatua ya maisha ya Kikristo. Nguvu ya neema ya Mungu inayookoa kwa njia ya imani (Waefeso 2:8) ni nguvu ile ile ya neema ya Mungu inayotakasa kupitia imani.




Comments