Nenda kwenye Karamu ya Bwana
- Dalvin Mwamakula
- Apr 28
- 1 min read
Updated: May 1

Onjeni mwone ya kuwa Bwana ni mwema! (Zaburi 34:8)
Kwa ninyi mnaosema hamjapata kuonja utukufu wa Mungu, nasema, mmeonja vichangamsha kinywa vingi.
Je, umewahi kutazama angani? Je, umewahi kukumbatiwa? Umewahi kukaa mbele ya joto la moto? Umewahi kutembea msituni, ukaketi kando ya ziwa, umelala kwenye bembea kwenye majira ya joto? Je, umewahi kunywa kinywaji chako ukipendacho siku ya joto au kula chochote kizuri?
Kila tamanio ni aidha mvuto wa ibada au mvuto uliopotoka unaoelekeza kwenye utukufu wa mbinguni.
Unasema hujaonja utukufu wa Mungu. Ninasema, umeonja vichamgamsha kinywa. Nenda kwenye chakula. Nenda kwa Mungu mwenyewe.
Umeona vivuli; angalia uhalisa. Umetembea katika miale ya joto ya mchana; geuka na uangalie jua lenyewe - ndiyo, kupitia lenzi ya ulinzi na yenye kunoa ya injili. Mmesikia mwangwi wa utukufu wa Mungu kila mahali; elekeza moyo wako kwa muziki asili.
Mahali pazuri pa kuuelekeza moyo wako ni kwenye msalaba wa Yesu Kristo. “Tumeuona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli” (Yohana 1:14).
Ikiwa unataka udhihirisho wa kina zaidi la utukufu wa Mungu, mtazame Yesu katika Injili, na uangalie hasa msalaba. Hilo litakazia macho yako na kurekebisha moyo wako na kuamsha vionjo vyako ili uweze kuona na kusikia na kuonja utukufu wa Mungu wa kweli kila mahali.
Hilo ndilo uliloumbwa kwa ajili yake. Ninakusihi: usitupe maisha yako kwenye vivuli. Mungu alikufanya uone na uonje ya utukufu wake. Fuatilia hilo kwa moyo wako wote na zaidi ya vitu vingine vyote. Umeonja vifungua kinywa. Sasa nenda kwenye karamu kamili.
Comentários