Nguvu kwa ajili ya Kufanya Mambo ya Leo
- Dalvin Mwamakula
- Jun 30
- 2 min read

Utimizeni wokovu wenu kwa kuogopa na kutetemeka, kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu kwa kulitimiza kusudi lake jema. (Wafilipi 2:12-13)
Mungu ndiye mtenda kazi mwenye maamuzi hapa. Utimizeni wokovu wenu kwa kuogopa na kutetemeka, kwa maana Mungu ndiye atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu. Mungu anataka na anafanya kazi kwa mapenzi yake mema. Lakini kuamini hivyo hakufanyi Wakristo ku kakaa kaakaa tu. Inawafanya kuwa na matumaini na nguvu na ujasiri.
Kila siku kuna kazi ya kufanywa katika huduma yetu ya pekee. Paulo anatuamuru tufanye kazi katika kutekeleza hayo. Lakini anatuambia jinsi ya kufanya hivyo kwa uwezo ambao Mungu hutoa: mwaminini Yeye! Amini ahadi kwamba katika siku hii Mungu atakuwa akifanya kazi ndani yako kutaka na kufanya kazi kwa mapenzi yake mema.
Nguvu tunazohitaji sasa na katika miongo ijayo zinatoka kwa Kristo mwenye nguvu, ambaye daima yupo kutenda kwa ajili ya mapenzi yake mema.
Ni Mungu mwenyewe, akifanya kazi kwa neema kila wakati, ambaye huleta ahadi ya neema ya wakati ujao katika uzoefu wetu wa sasa. Sio shukrani kwa ajili ya neema iliyopita ambayo Paulo anazingatia wakati anaelezea jinsi tunavyo utimiza wokovu wetu. Ninataja hili kwa sababu tu Wakristo wengi, wakiulizwa nini nia ya utii, watasema shukrani. Lakini hivyo sivyo Paulo anasisitiza anapozungumza kuhusu nia na nguvu kwa ajili ya kazi yetu. Anakazia imani katika yale ambayo Mungu bado atafanya, sio yale ambayo amefanya tu. Utimize wokovu wako! Kwanini? Kivipi? Kwa maana kuna neema mpya kwa kila dakika kutoka kwa Mungu. Yeye yuko kazini kwenye nia yako na kufanya kwako kila wakati unapotia nia na kufanya. Amini hilo kwa changamoto za saa ijayo na miaka elfu iijayo.
Nguvu ya neema ya wakati ujao ni nguvu ya Kristo aliye hai - daima ipo ili kufanya kazi kwa ajili yetu katika kila wakati ujao tunaoingia. Kwa hiyo Paulo anapoeleza matokeo ya neema ya Mungu iliyokuwa pamoja naye, anasema, “Sitathubutu kusema lolote isipokuwa lile ambalo Kristo alilolitimiza kwa kunitumia mimi kuwaleta Mataifa kwenye utii – kwa neno na kwa tendo” (Warumi 15:18).
Kwa hiyo, kwa kuwa asingethubutu kusema juu ya kitu chochote isipokuwa kile ambacho Kristo alikamilisha kupitia huduma yake, na bado alizungumza juu ya neema iliyotimiza kupitia huduma yake (1 Wakorintho 15:10), hii lazima inamaanisha kwamba nguvu ya neema ni nguvu ya Kristo.
Ambayo ina maana kwamba nguvu tunayohitaji kwa dakika tano zijazo na miongo mitano ijayo ya huduma ni neema ya baadaye ya Kristo mwenye nguvu, ambaye daima atakuwepo kwa ajili yetu - tayari kufanya kazi kwa ajili ya mapenzi yake mema.




Comments