top of page

Ni Maombi ya Namna Gani Humpendeza Mungu?

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • May 29
  • 2 min read
ree

“Huyu ndiye nitakayemwangalia: yeye aliye mnyenyekevu na mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.” (Isaya 66:2)


Alama ya kwanza ya moyo mnyoofu ni kwamba hutetemeka usikiapo neno la Bwana. 

 

Isaya 66 inazungumzia tatizo la baadhi ya wanaoabudu kwa njia inayompendeza Mungu na wengine wanaoabudu kwa njia isiyompendeza. Mstari wa 3 unaeleza waovu wanaoleta dhabihu zao, “Achinjaye ng’ombe ni kama ule amwuaye mtu.” Sadaka zao ni chukizo kwa Mungu - sawa na mauaji. Kwanini? 

 

Katika mstari wa 4 Mungu anaeleza, “Nilipoita, hakuna aliyeitikia, niliposema, hawakusikia.” Sadaka zao zilikuwa machukizo kwa Mungu kwa sababu watu walikuwa viziwi kwa sauti yake. Lakini vipi kuhusu wale ambao Mungu alisikia sala zao? Mungu anasema katika mstari wa 2, “Huyu ndiye nitakayemwangalia: yeye aliye mnyenyekevu na mwenye roho iliyopondeka, na atetemekaye chini ya neno langu. 

 

Ninahitimisha kutokana na hili kwamba alama ya kwanza ya wanyoofu, ambao sala zao ni furaha kwa Mungu, ni kwamba wanatetemeka chini ya neno la Mungu. Hawa ndio watu ambao Bwana atawatazama. 


Alama ya kwanza ya wanyoofu, wenye sala zinazompendeza Mungu, ni kutetemeka chini ya neno la Mungu. Hawa ndio anaowatazama Bwana.

 

Hivyo basi, sala ya mtu mwadilifu inayompendeza Mungu hutoka kwenye moyo ambao mwanzoni hujihisi kuwa katika hali ya hatari mbele za Mungu. Unatetemeka isikiapo neno la Mungu, kwa sababu unahisi kuwa mbali sana na kiwango cha Mungu, uko wazi mbele ya hukumu yake, hauna msaada wowote, na una huzuni kwa sababu ya mapungufu yake.

 

Hivi ndivyo alivyosema Daudi katika Zaburi 51:17, “Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.” Kitu cha kwanza kinachofanya sala ikubalike kwa Mungu ni moyo uliovunjika na unyenyekevu wa yule anayeomba. Wanatetemeka chini ya neno lake.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page