top of page

Nikiwa Na Wasiwasi

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Nov 14
  • 2 min read
ree

. . . Mtwikeni yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana na mambo yenu. (1 Petro 5:7)

 

Kuna ahadi inayofaa kwa kila dhambi unayojaribiwa kuifanya na kila aina ya kutoamini ambayo inakuweka mbali na kukufanya uwe na wasiwasi. Kwa mfano:

 

Wakati nina wasiwasi ya kupata ugonjwa na kuumwa, ninapigana na kutoamini kwa ahadi, "Mateso ya mwenye haki ni mengi, lakini Bwana humponya nayo yote" (Zaburi 34:19). Na ninaipokea ahadi hiyo kwa kutetemeka, “nikijua ya kuwa mateso huleta saburi, na saburi huleta uthabiti, na uthabiti huleta tumaini, na tumaini halitukatishi tamaa; kwa sababu Mungu amekwisha kumimina pendo lake mioyoni mwetu kwa nlia ya Roho Mtakatifu ambaye ametupatia” (Warumi 5:3–5).

 

 

Ninapokuwa na wasiwasi juu ya kufa, ninapambana na kutoamini kwa ahadi kwamba “hakuna hata mmoja wetu anayeishi kwa ajili yake mwenyewe, na hakuna hata mmoja wetu anayekufa kwa ajili yake mwenyewe. Kwa maana tukiishi, twaishi kwa Bwana, na tukifa, twafa kwa Bwana. Basi, kama tukiishi au tukifa, sisi ni wa Bwana. Kwa maana Kristo alikufa kwa ajili hiyo, akaishi tena, ili wapate kuwa Bwana wa waliokufa na walio hai pia” (Warumi 14:7–9).

 

Ninapokuwa na wasiwasi ili nivunjike imani na kuanguka kutoka kwa Mungu, ninapambana na kutokuamini kwa ahadi, “Yeye aliyeanza kazi njema ndani yenu ataimaliza hata siku ya Yesu Kristo” (Wafilipi 1:6); na, “Aweza kuwaokoa kabisa wao wamkaribiao Mungu kwa yeye, maana yu hai siku zote ili kuwaombea” (Waebrania 7:25). 

 

Kwa hiyo, tufanye vita, sio na watu wengine, bali na kutokuamini kwetu wenyewe.

Ni mzizi wa wasiwasi, ambao, mara nyingi, ni mzizi wa dhambi nyingine nyingi. 

 

Kwa hiyo, na tukazie macho kwenye ahadi za Mungu zenye thamani na kuu sana. Chukua Biblia, mwombe Roho Mtakatifu akusaidie, weka ahadi moyoni mwako, na pigana vita vizuri - kuishi kwa imani katika neema ya wakati  ujao.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page