Ninaweza Kuridhika Katika Kila Hali
- Dalvin Mwamakula
- May 29
- 2 min read

Nimejifunza katika hali yoyote niliyo nayo kuridhika. Najua kupungukiwa, na najua kufanikiwa. Katika hali yoyote na katika kila hali, nimejifunza siri ya kushiba na njaa, wingi na uhitaji. Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu. (Wafilipi 4:11-13)
Utoaji wa neema ya Mungu ya siku hadi siku wa wakati ujao unamwezesha Paulo kushiba au kuwa na njaa, kufanikiwa au kuteseka, kuwa na utele au kupungukiwa.
“Naweza kufanya mambo yote” kwa kweli humaanisha “mambo yote,” sio mambo rahisi tu. “Mambo yote” maana yake, “Kwa njia ya Kristo ninaweza kuona njaa na kuteseka na kuhitaji. Hilo laweka ahadi yenye kushangaza ya Wafilipi 4:19 katika nuru sahihi: “Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.”
Je, “kila hitaji lenu” linamaanisha nini katika mtazamo wa Wafilipi 4:11–12? Inamaanisha “yote unayohitaji ili utosheke kwa kumtukuza Mungu.” Ambayo inaweza kujumuisha nyakati za njaa na uhitaji. Upendo wa Paulo kwa Wafilipi ulitiririka kutokana na kuridhika kwake katika Mungu, na kuridhika kwake kulitiririka kutokana na imani yake katika neema ya wakati ujao ya utoaji wa Mungu usio na dosari kuwa yote aliyohitaji wakati wa kushiba na kuhitaji.
Imani katika ahadi hii— “Sitakuacha kamwe”— inavunja nguvu zote ambazo zinamvunjia Mungu heshima —tamaa zote.
Ni dhahiri basi kwamba tamaa ni kinyume kabisa cha imani. Ni kupoteza kuridhika ndani ya Kristo ili tuanze kutamani mambo mengine ili kutosheleza matamanio ya mioyo yetu ambayo uwepo wa Mungu pekee ndio unaweza kutosheleza. Na hakuna kukosea kwamba vita dhidi ya tamaa ni vita dhidi ya kutoamini ahadi ya Mungu kuwa yote tunayohitaji katika kila hali.
Hili liko wazi sana katika Waebrania 13:5. Tazama jinsi mwandishi anavyoleta hoja kuhusu uhuru wetu kutoka kwa kupenda pesa - uhuru kutoka kwa kutamani - uhuru wa kutosheka katika Mungu: "Wekeni maisha yenu bila kupenda pesa, na kuridhika na vitu mlivyo navyo, kwa maana yeye amesema, kamwe sitakuacha wala kukutupa.’” Imani katika ahadi hii— “Sitakuacha kamwe”—inavunja nguvu zote ambazo zinamvunjia Mungu heshima—tamaa zote.
Wakati wowote tunapohisi kuongezeka kidogo kwa tamaa ndani ya mioyo yetu, lazima tugeuke na kupigana nayo kwa nguvu zetu zote kwa kutumia silaha za imani hii.




Comments