top of page

Ninawezaje Kujazwa na Roho?

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Feb 26
  • 2 min read

Yote yaliyoandikwa zamani yaliandikwa kwa ajili ya mafundisho yetu, ili kwa uvumilivu na faraja ya Maandiko tuwe na tumaini. (Warumi 15:4)

 

Tunawezaje kujazwa na Roho Mtakatifu? Tunawezaje kupata uzoefu wa kumwagwa kwa Roho Mtakatifu juu ya kanisa letu na sisi wenyewe ambako kunatufanya tuwe na furaha isiyozuilika na kutuweka huru, na kutupa nguvu za kuwapenda wale walio karibu nasi kwa njia za kweli kiasi kwamba wanakuja kwa Kristo? 


Jibu: Tafakari mchana na usiku juu ya ahadi za Mungu zisizo na kifani, zinazotoa tumaini. Kama Warumi 15:4 inavyotuonyesha, hivyo ndivyo Paulo alivyotunza moyo wake ukiwa umejaa tumaini, furaha, na upendo. "Kwa kuwa yote yaliyoandikwa zamani yaliandikwa kwa ajili ya mafundisho yetu, ili kwa uvumilivu na faraja ya Maandiko tupate kuwa na tumaini." 


Ni neno la ahadi linalotujaza tumaini, linalotupa furaha inayofurika kwa nguvu na uhuru wa kumpenda jirani yetu. Huu ndio ukamilifu wa Roho Mtakatifu.

Uhakika kamili wa tumaini unatokana na kutafakari ahadi za neno la Mungu. Na hili halipingani na mistari tisa mbele inaposema kwamba Roho Mtakatifu anatupa tumaini (Warumi 15:13). Hii ni kwa sababu Roho Mtakatifu ndiye mwandishi wa kiungu wa Maandiko. Neno lake ndilo njia ya kazi yake. Haina kupingana kwamba njia anayotumia kutujaza na tumaini ni kwa kutujaza neno lake la ahadi. 


Tumaini si hisia isiyoeleweka inayotokea tu kutoka mahali popote, kama maumivu ya tumbo. Tumaini ni ujasiri kwamba mustakabali wa ajabu ulioahidiwa kwetu na neno la Roho utatimia kweli. Kwahiyo, njia ya kujazwa na Roho ni kujazwa na neno lake. Njia ya kuwa na nguvu za Roho ni kuamini ahadi za neno lake. 


Kwa maana ni neno la ahadi linalotujaza tumaini, na tumaini linatupa furaha, na furaha inafurika katika nguvu na uhuru wa kumpenda jirani yetu. Na huo ndiyo ukamilifu wa Roho Mtakatifu.



Comentarios


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page