Nitaridhika Lini?
- Dalvin Mwamakula
- Jun 30
- 2 min read

“Nimefanya jina lako lijulikane kwao, nami nitaendelea kufanya lijulikane kwao, ili upendo ule unaonipenda mimi uwe ndani yao na mimi mwenyewe nipate kuwa ndani yao.” (Yohana 17:26)
Hebu fikiria kuweza kufurahia kile kinachofurahisha zaidi kwa nguvu na shauku isiyo na mipaka, inayozidi kuongezeka milele.
Kwa sasa, hii siyo hali yetu. Mambo matatu yanasimama kama kizuizi dhidi ya kuridhika kwetu kikamilifu katika ulimwengu huu:
Hakuna kitu katika ulimwengu huu chenye thamani binafsi kubwa kiasi cha kukidhi matamanio ya ndani kabisa ya mioyo yetu.
Hatuna nguvu ya kufurahia hazina bora kwa kadiri ya thamani yake kamili.
Furaha yetu katika vitu vya hapa duniani hufikia mwisho. Hakuna kinachodumu.
Lakini ikiwa lengo la Yesu katika Yohana 17:26 litatimia, yote haya yatabadilika. Anasali kwa Baba yake kutuhusu,
“Nimefanya jina lako lijulikane kwao nami nitaendelea kufanya lijulikane, ili upendo ule unaonipenda mimi uwe ndani yao na mimi mwenyewe nipate kuwa ndani yao.”
Mungu hampendi Mwanae jinsi anavyowapenda wenye dhambi. Anampenda Mwanae kwa sababu Mwana anastahili kupendwa sana. Yaani anampenda Mwanae kwa sababu Mwana ni mzuri sana. Hii inamaanisha kwamba upendo huu ni furaha kamili. Yesu anaomba kwamba furaha hii ambayo Mungu anayo katika Mwanawe iwe ndiyo furaha ileile ambayo sisi tunayo katika Mwana.
Ikiwa furaha ya Mungu katika Mwana itakuwa furaha yetu, basi kile tunachofurahia, Yesu, kitakuwa na thamani binafsi isiyokwisha. Kamwe hatakuwa wa kuchosha au kukatisha tamaa au kusababisha msongo. Hakuna hazina kubwa zaidi inayoweza kufikiriwa kuliko Mwana wa Mungu.
Lakini ongeza juu ya hili kile ambacho Yesu anaombea; yaani, kwamba uwezo wetu — nguvu zetu, shauku yetu — wa kufurahia hazina hii isiyokwisha hautazuiwa na udhaifu wa kibinadamu.
Tutamfurahia Mwana wa Mungu kwa furaha ileile ya Baba yake mwenye uweza wote.
Furaha ya Mungu katika Mwana itakuwa ndani yetu na itakuwa yetu. Na hii furaha haitakoma kamwe, kwa sababu Baba wala Mwana hawatakoma kamwe. Upendo wao kwa kila mmoja utakuwa upendo wetu kwao, na hivyo kuwapenda kwetu hakutakufa kamwe.




Comments