Njia Mbili za Kumkumbuka Yesu
- Dalvin Mwamakula
- Mar 31
- 2 min read

"Wapendeni adui zenu na waombeeni wanaowatesa ninyi." (Mathayo 5:44)
Mkumbuke Yesu Kristo, aliyefufuka kutoka kwa wafu, uzao wa Daudi, kama ilivyohubiriwa katika Injili yangu. (2 Timotheo 2:8)
Paulo anataja njia mbili mahususi za kumkumbuka Yesu: Mkumbuke kama amefufuka kutoka kwa wafu. Na mkumbuke kuwa ni uzao wa Daudi. Kwanini ukumbuke mambo haya mawili kuhusu Yesu?
Kwa sababu ikiwa amefufuka kutoka kwa wafu, yuko hai na ameshinda kifo — ikiwemo kifo chetu! “Ikiwa Roho wake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu” (Warumi 8:11).
Hii inamaanisha kwamba haijalishi mateso yanakuwa makubwa kiasi gani, baya zaidi ambalo linaweza kufanyika hapa duniani ni kukuua. Na Yesu ameondoa uchungu kutoka kwa adui huyo. Yuko hai. Nawe utakuwa hai. "Usiwaogope wale wanaoua mwili lakini hawawezi kuiua roho" (Mathayo 10:28).
Haijalishi ukali wa mateso, baya zaidi la kutokea duniani ni kifo, lakini Yesu ameondoa uchungu wa kifo. Yuko hai, nawe utakuwa hai.
Lakini zaidi ya hayo, ufufuo wa Yesu haukuwa ufufuo wa kawaida. Ilikuwa ni ufufuo wa mwana wa Daudi. "Mkumbuke Yesu Kristo, aliyefufuka katika wafu, uzao wa Daudi." Kwanini Paulo anasema hivyo?
Kwa sababu kila Myahudi alijua maana yake. Hiyo ilimaanisha kwamba Yesu ndiye Masihi (Yohana 7:42). Na hilo lilimaanisha kwamba ufufuo huu ulikuwa ufufuo wa Mfalme wa milele. Sikiliza maneno ya malaika kwa Mariamu, mama yake Yesu:
“Tazama, utapata mimba na kuzaa mtoto wa kiume, nawe utamwita jina lake Yesu. Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Aliye Juu Zaidi. Na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake, naye atatawala juu ya nyumba ya Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho. (Luka 1:31-33)
Kwa hiyo, mkumbuke Yesu, unayemtumikia, na unayeteseka kwa ajili yake. Yeye hayuko hai kutoka kwa wafu pekee, lakini yuko hai kama Mfalme ambaye atatawala milele - ufalme wake hautakuwa na mwisho. Haijalishi wanakufanyia nini, huna haja ya kuogopa. Utaishi tena. Pia, utatawala pamoja naye.




Comments