top of page

Njia Sita Yesu Alipambana na Hali ya Kuhisi Sonona

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Jun 30
  • 2 min read
ree

Akamchukua Petro pamoja na wale wana wawili wa Zebedayo, akaanza kuhuzunika na kufadhaika. (Mathayo 26:37)


Biblia inatupa mtazamo wa kustaajabisha katika nafsi ya Yesu usiku kabla ya kusulubiwa kwake. Tazama na ujifunze kutokana na jinsi Yesu alivyopigana vita vyake vya kimkakati dhidi ya kukata tamaa au sonona.


  1. Alichagua marafiki wa karibu wa kuwa naye. "Akichukua pamoja naye Petro na wana wawili wa Zebedayo" (Mathayo 26:37).


  2. Alifungua nafsi yake kwao. Akawaambia, “Nafsi yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa” (Mathayo 26:38).


  3. Aliomba maombezi kutoka kwao na ushirikiano katika vita. “Kaeni hapa, mkeshe pamoja nami” (Mathayo 26:38).


  4. Alimimina moyo wake kwa Baba yake katika sala. "Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki kiniondeke" (Mathayo 26:39).


  5. Aliipumzisha roho yake katika hekima kuu ya Mungu. "Walakini, si kama nipendavyo mimi, bali kama upendavyo wewe" (Mathayo 26:39).


  6. Alikazia jicho lake kwenye neema tukufu ya wakati ujao iliyokuwa inamngoja upande wa pili wa msalaba. “Kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba, bila kujali aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu” (Waebrania 12:2).


Kitu kinapoanguka maishani mwako ambacho kinaonekana kutishia wakati wako ujao, kumbuka hili: Mawimbi ya kwanza ya bomu moyoni mwako, kama yale ambayo Yesu alihisi akiwa Gethsemane, sio dhambi. Hatari ya kweli ni kujisalimisha kwao. Kujisalimisha au kukubali kushindwa. Kutokupigana vita vya kiroho. Na mzizi wa kujisalimisha huko kwa dhambi ni kutoamini - kushindwa kupigania imani ya neema ya wakati ujao. Kushindwa kuthamini yote ambayo Mungu ameahidi kuwa kwa ajilio yetu katika Yesu.


Katika Gethsemane Yesu anatuonyesha njia nyingine. Sio isiyo na uchungu, na sio batili. Mfuate Yeye. Tafuta marafiki zako wa kiroho unaowaamini. Fungua roho yako kwao. Waombe kukesha pamoja nawe na kuomba. Imimine nafsi yako kwa Baba. Tulia katika hekima kuu ya Mungu. Na kazia macho yako juu ya furaha iliyowekwa mbele yako katika ahadi kuu na za thamani za Mungu.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page