top of page

Nuru Zaidi ya Nuru

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Apr 28
  • 2 min read

Updated: May 1

Basi ikiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Yafikirini mamba yaliyo juu, wala si ya duniani. (Wakolosai 3:1-2)

 

Yesu Kristo anaburudisha. Kwa hiyo, tafuteni mambo yaliyo juu. Usimbadilishe Kristo likizo hii na mambo madogo madogo. Kukimbia kutoka kwa Kristo hadi kwenye tafrija isiyo ya Kristo huleta ukamwe wa nafsi.

 

Mara ya kwanza inaweza kuhisi kama uhuru na furaha kuacha kuomba na kulipuuza Neno. Lakini hatimaye tunalipa gharama: kutokuwa na kina, kutokuwa na nguvu, kuathirika kwa dhambi, kujishughulisha na mambo madogo madogo, mahusiano ya juu juu, na upotevu wa kutisha wa kupoteza shauku ya ibada na mambo ya Roho.

 

Usiruhusu ujio wa likizo ifanye roho yako kusinyaa. Mungu aliumba likizo kama kionjo cha mbinguni, sio mbadala.

 

Msambazaji barua akikuletea barua ya mapenzi kutoka kwa mchumba wako, usimtamani msambazaji wa barua. Usikipende kipande cha video na ujikute wewe mwenyewe  kuwa huwezi kupenda ukweli ujao.

 

Yesu Kristo ndiye kitovu chenye kuburudisha cha kiangazi. Yeye ni mkuu katika mambo yote (Wakolosai 1:18), ikijumuisha likizo na pikiniki na mpira wa mikono na matembezi marefu na kupika. Anatualika wakati huu wa kiangazi, “Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha” (Mathayo 11:28).

 

Je, tunaitaka? Hilo ndilo swali.


Kristo anajitoa kwetu kadri ya jinsi tunavyotaka burudisho kutoka kwake. “Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote”

 

Neno la Petro kwetu kuhusu hili ni, “Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, nyakati za kuburudishwa zaja  kutoka uwepo wa Bwana” (Matendo 3:19–20). Toba sio tu kugeuka kutoka kwa dhambi, lakini pia kumgeukia Bwana kwa mioyo iliyo wazi na inayotarajia na kunyenyekea.

 

Je, huu ni mtazamo wa aina gani wa kiangazi? Ni mawazo ya Wakolosai 3:1-2, “Basi ikiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Yafikirini mambo yaliyo juu, wala si ya duniani.”

 

Ni dunia ya Mungu! Ni hakikisho la video la uhalisi wa jinsi majira ya kiangazi ya milele yatakavyokuwa wakati “mji huo hauna haja ya jua wala mwezi kuuangazia, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo” (Ufunuo. 21:23).

 

Jua la kiangazi ni kielelezo tu cha jua litakalokuwa: utukufu wa Mungu. Kiangazi ni ya kuona na kutuonyesha hilo. Je! unataka kuwa na macho ya kuona? Bwana, turuhusu tuone nuru zaidi ya nuru.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page