top of page

Pale Wote Watakapokuacha

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Feb 26
  • 2 min read
ree

Katika utetezi wangu wa kwanza, hakuna mtu aliyekuja kusimama nami, bali wote waliniacha. Na isiweze kuhesabiwa dhidi yao! Lakini Bwana alisimama nami na kunitia nguvu, ili kupitia mimi ujumbe uweze kutangazwa kikamilifu na mataifa yote wapate kuusikia. Kwahiyo niliokolewa kutoka katika kinywa cha simba. Bwana ataniokoa kutoka katika kila tendo ovu na kunileta salama katika ufalme wake wa mbinguni. Utukufu uwe kwake milele na milele. Amina. (2 Timotheo 4:16–18)

 

Asubuhi ya leo nilikuwa nikitafakari maneno haya mazuri na yenye kuhuzunisha. Paulo yuko kizuizini huko Roma. Kwa tunavyojua, hakuwahi kuachiliwa. Barua yake ya mwisho inaishia hivi. 

 

Fikiria na ushangazwe!

 

Ameachwa: “hakuna aliyekuja kusimama nami.” Yeye ni mzee. Mtumishi mwaminifu. Katika mji wa kigeni, mbali na nyumbani. Amezungukwa na maadui. Katika hatari ya kifo. Kwanini? Jibu: Ili aweze kuandika sentensi hii ya thamani kwa ajili ya nafsi zetu zilizokatishwa tamaa, au zenye hofu, au zenye upweke: “Lakini Bwana alisimama nami!”

 

Ah, jinsi gani nayapenda maneno hayo! Unapoachwa na marafiki wa karibu, je, unalia dhidi ya Mungu? Je, watu katika maisha yako, basi, ndio mungu wako kweli? Au unapata ujasiri katika ukweli huu mzuri: “Niko pamoja nawe daima, hadi mwisho wa nyakati” (Mathayo 28:20) — bila kujali nani ana kukimbia? Je, unaupa moyo wako nguvu kwa kiapo hiki kisichoweza kubadilika: “Sitakuacha wala sitakupungukia” (Waebrania 13:5)? 

 

Basi na tuseme, “Bwana alisimama nami!”


Unapoachwa na marafiki, Je, unalia dhidi ya Mungu au unapata ujasiri katika ukweli kwamba Mungu yuko pamoja nawe daima? Je, unatiwa moyo na kiapo chake: “Sitakuacha wala sitakupungukia”?

 

Swali: Ni nini kilitishiwa katika 2 Timotheo 4:18? Jibu: kwamba Paulo asingeweza kufikia ufalme wa mbinguni wa Bwana! Lakini dhidi ya tishio hilo Paulo analia, “Bwana atanileta salama katika ufalme wake wa mbinguni.”

 

Swali: Je, kufika kwa Paulo kwenye ufalme wa mbinguni kulitishiwa vipi? Jibu: “matendo maovu.” “Bwana ataniokoa kutoka katika kila tendo ovu na kunileta salama katika ufalme wake wa mbinguni.”

 

Swali: Je, tendo ovu lingewezaje kutishia kufika kwa Paulo kwenye ufalme wa mbinguni? Jibu: kwa kumjaribu kuacha utii wake kwa Kristo kupitia kutotii.

 

Swali: Je, jaribu hili lilikuwa “kinywa cha simba” ambalo alikombolewa kutoka kwalo? Jibu: Ndio. "Adui yako, shetani, huzunguka kama simba angurumaye, akitafuta mtu wa kummeza. Mpingeni, mkisimama imara katika imani yako (1 Petro 5:8-9).

 

Swali: Kwahiyo, ni nani anapata utukufu kwamba Paulo hakusalimu amri kwa jaribu hili la kishetani, bali ali stahimili hadi mwisho katika imani na utiifu? Jibu: “Kwake [Bwana] utukufu na mamlaka una Yeye milele na milele” (1 Petro 5:10). "Utukufu uwe kwake milele na milele. Amina" (2 Timotheo 4:18).

 

Swali: Kwanini? Je, hakuwa Paulo aliyesimama imara? Jibu: "Bwana alisimama nami na kunitia nguvu!"

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page