top of page

Panga kwa ajili ya Maombi

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Oct 7
  • 2 min read
ree

“Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. Kwa hili Baba yangu hutukuzwa, kwa vile mzaapo matunda mengi na hivyo kuwa wanafunzi wangu. . . . Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu ikamilike. (Yohana 15:7–8,11)

 

Sala hufuata furaha katika ushirika wenye kuzaa matunda na Yesu, tukijua kwamba Mungu hutukuzwa tunapozaa matunda kama majibu ya maombi. Kwanini watoto wa Mungu mara nyingi hushindwa kuwa na mazoea thabiti ya maombi yenye furaha, yenye matunda?

 

Labda kama sijakosea sana, moja ya sababu sio kwamba hatutaki, bali hatupangi.

 

Ikiwa unataka kuchukua likizo ya wiki nne, hauamki tu asubuhi moja ya kiangazi na kusema, "Hebu, twende leo!" Hutakuwa na chochote tayari. Hutajua pa kwenda. Hakuna kilichopangwa.

 

Lakini ndivyo wengi wetu wanavyochukulia maombi. Tunaamka siku baada ya siku na kutambua kwamba nyakati muhimu za maombi zinapaswa kuwa sehemu ya maisha yetu, lakini hakuna kitu kilicho tayari.


Hatuombi si kwasababu hatutaki kuomba. Hatuombi kwasababu hatupangi kuomba. Matokeo ya kutokupanga kuomba ni kurudia yale yale ya zamani.

 

Hatujui pa kwenda. Hakuna kilichopangwa. Hakuna muda. Hakuna eneo. Hakuna utaratibu. Na sote tunajua kwamba kinyume cha kupanga sio mtiririko mzuri wa ghafla, na wa kina, wa matukio katika maombi. Kinyume cha kupanga ni kurudia yale yale ya zamani.

 

Ikiwa hutapanga likizo, labda utakaa nyumbani na kutazama TV. Mtiririko wa kawaida na usio pangwa wa maisha ya kiroho hushuka hadi kiwango cha chini kabisa cha uhai. Kuna mbio za kukimbia na vita vya kupigana. Ikiwa unataka kufanywa upya katika maisha yako ya maombi, lazima upange kuyaona.

 

Kwa hiyo, himizo langu rahisi ni hili: Hebu tuchukue muda huu leo kufikiria upya vipaumbele vyetu na jinsi maombi yanavyofaa. Fanya azimio jipya. Jaribu mradi mpya na Mungu. Tenga muda. Tenga eneo. Chagua sehemu ya Maandiko ili kukuongoza.

 

Usitawaliwe na msongo wa siku zenye shughuli nyingi. Sote tunahitaji marekebisho ya katikati ya safari. Fanya hii iwe siku ya kugeukia maombi — kwa utukufu wa Mungu na kwa ukamilifu wa furaha yako.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page