top of page

Pumziko la Mwisho la Nafsi

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Sep 2
  • 1 min read
ree

Neno moja nimeomba kwa Bwana, ndilo nitakalolitafuta, nikae nyumbani mwa Bwana siku zote za maisha yangu, niutazame uzuri wa Bwana, na kutafakari hekaluni mwake. (Zaburi 27:4)

 

Mungu si mwenye kutokutoa mwitikio kwa shauku ya moyo uliomnyenyekevu. Anakuja na kuinua mzigo wa dhambi na kujaza mioyo yetu furaha na shukrani. “Umegeuza maombolezo yangu kuwa kucheza; umenivua gunia na kunivika furaha, ili utukufu wangu ukuimbie sifa zako na usinyamaze. Ee Bwana, Mungu wangu, nitakushukuru milele!” (Zaburi 30:11-12).

 

Lakini,


Furaha yetu haiinuki tu kutoka katika mtazamo wa kipindi cha nyuma kwa shukrani. Huinuka pia kutoka katika mtazamo wa mbele kwa matumaini.

"Kwa nini unashuka moyo, Ee nafsi yangu, na kwa nini unafadhaika ndani yangu? Mtumaini Mungu; kwa maana nitamsifu tena, wokovu wangu na Mungu wangu” (Zaburi 42:5–6).

 

“Nimemngoja Bwana, nafsi yangu inamngoja, na neno lake nalitumainia” (Zaburi 130:5).

 

Mwishowe, moyo hautamani zawadi yoyote nzuri ya Mungu, lakini Mungu mwenyewe. Kumwona na kumjua na kuwa mbele yake ni karamu ya mwisho ya roho. Zaidi ya hii hakuna utafutaji. Maneno hushindwa. Tunaiita raha, furaha, shangwe. Lakini hivi ni viashiria dhaifu vya uzoefu usioelezeka:

 

“Neno moja nimeomba kwa BWANA, ndilo nitakalolitafuta, nikae nyumbani mwa BWANA siku zote za maisha yangu, niutazame uzuri wa BWANA, na kutafakari hekaluni mwake” (Zaburi 27:4).

 

“Mbele ya uwepo wako kuna furaha tele; mkono wako wa kuume kuna mema ya milele” (Zaburi 16:11).

 

"Jifurahishe katika Bwana" (Zaburi 37:4).

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page