Rehema ya Mungu yenye Hekima
- Dalvin Mwamakula
- Sep 30
- 1 min read

Tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa, kikwazo kwa Wayahudi na kwa watu wa mataifa ni upumbavu, lakini kwa wale walioitwa, Wayahudi na Wagiriki, Kristo ni nguvu ya Mungu na hekima ya Mungu. (1 Wakorintho 1:23–24)
Juu ya habari za kutisha kwamba tumeanguka chini ya hukumu ya Muumba wetu na kwamba amefungwa na tabia yake ya haki ili kuhifadhi thamani ya utukufu wake kwa kumimina ghadhabu ya milele juu ya dhambi zetu, kuna habari ya ajabu ya injili.
Hii ni kweli ambayo hakuna mtu anaweza kujifunza kutoka kwa asili. Ukweli wa injili unapaswa kuambiwa kwa majirani na kuhubiriwa makanisani na kubebwa na wamisionari.
Habari njema ni kwamba Mungu mwenyewe ameamuru njia ya kutosheleza matakwa ya haki yake bila kushutumu jamii yote ya kibinadamu.
Kuzimu ni njia mojawapo ya kusuluhisha hesabu na wenye dhambi na kudumisha haki yake. Lakini kuna njia nyingine. Mungu alitoa njia nyingine. Hii ni injili.
Hekima ya Mungu imeweka njia kwa ajili ya upendo wa Mungu kutukomboa kutoka katika ghadhabu ya Mungu bila kuathiri haki ya Mungu. Hiyo hapo. Injili. Hebu niseme tena polepole: Hekima ya Mungu imeweka njia kwa ajili ya upendo wa Mungu kutukomboa kutoka katika ghadhabu ya Mungu bila kuathiri haki ya Mungu.
Na hekima hii ni nini? Kifo cha Mwana wa Mungu kwa ajili ya wenye dhambi! “Sisi tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa . . . nguvu za Mungu na hekima ya Mungu” (1 Wakorintho 1:23–24).
Kifo cha Kristo ni hekima ya Mungu kwamba upendo wa Mungu huwaokoa wenye dhambi kutoka katika ghadhabu ya Mungu, huku ukishikilia na kudhihirisha haki ya Mungu katika Kristo.




Comments