top of page

Sababu Tano kwanini Kifo Ni Faida

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Nov 14
  • 2 min read
ree

Kwa maana kuishi kwangu ni Kristo, na kufa ni faida. (Wafilipi 1:21)

 

Je, ni kwa namna gani "kufa ni faida"?

 

  1. Roho zetu zitakamilishwa (Waebrania 12:22–23).


Lakini ninyi mmekuja mlima Sayuni, Yerusalemu ya mbinguni, mji wa Mungu aliye hai. Mmekuja penye kusanyiko kubwa la malaika maelfu kwa maelfu wasiohesabika, na mkutano wa wazaliwa wa kwanza ambao majina yao yameandikwa mbinguni na kwa Mungu, mhukumu wa watu wote; kwenye roho za wenye haki waliokamilishwa .

 

Hakutakuwa na dhambi tena ndani yetu. Tutamaliza vita vya ndani na kukatishwa tamaa kwa moyo kwa kumchukiza Bwana ambaye alitupenda na akutoa uhai wake kwa ajili yetu.

 

  1. Tutaondolewa maumivu ya ulimwengu huu (Luka 16:24–25).

 

Furaha ya ufufuo haitakuwa yetu bado, lakini furaha ya uhuru kutoka kwa maumivu itakuwa yetu. Yesu anasimulia hadithi ya Lazaro na yule tajiri ili kuonyesha mabadiliko makubwa yanayokuja wakati wa kifo.

 

“[Yule tajiri] akapaza sauti, ‘Baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake katika maji, auburudishe ulimi wangu, kwa maana ninateseka katika moto huu. Lakini Ibrahimu akasema, Mwana, kumbuka ya kuwa wewe ulipokea mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo hivyo uliyapokea mabaya; lakini sasa yeye anafarijiwa hapa, nawe unataabika.’”

 

"Kwa maana kuishi kwangu ni Kristo, na kufa ni faida." Wafilipi 1:21

  1. Tutapewa pumziko la kina katika nafsi zetu (Ufunuo 6:9–11).

 

Kutakuwa na utulivu chini ya jicho na utunzaji wa Mungu ambao unashinda kitu chochote ambacho tumejua hapa katika jioni yenye hewa nyororo karibu na ziwa lenye amani zaidi katika nyakati zetu za furaha zaidi.

 

Nikaona chini ya madhabahu roho za wale waliouawa kwa ajili ya neno la Mungu na kwa ajili ya ushahidi waliokuwa wametoa. Wakilia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Bwana, mtakatifu na wa kweli, hata lini utahukumu na kulipiza kisasi damu yetu juu ya hao wakaao juu ya nchi? Kisha wakapewa kila mmoja vazi jeupe na kuambiwa wapumzike kidogo zaidi .

 

  1. Tutapata uzoefu wa ndani wa utulivu wa nyumbani (2 Wakorintho 5:8).

 

Ndiyo, tuna moyo wa ujasiri, na ni afadhali tuwe mbali na mwili na nyumbani kwa Bwana.

 

Jamii yote ya wanadamu inatamani nyumbani kwa Mungu, bila kujua. Tunapoenda nyumbani kwa Kristo, kutakuwa na kutosheka zaidi ya hali yoyote ya usalama na amani ambayo tumewahi kujua.

 

  1. Tutakuwa pamoja na Kristo (Wafilipi 1:21–23).

 

Kristo ni mtu wa ajabu kuliko mtu yeyote duniani. Yeye ni mwenye busara zaidi, mwenye nguvu, na mkarimu kuliko mtu yeyote unayefurahiya kukaa naye. Anavutia bila mwisho. Anajua hasa la kufanya na nini cha kusema kila wakati ili kuwafurahisha wageni wake kadiri wawezavyo kufurahi. Anafurika katika upendo na ufahamu usio na kikomo wa jinsi ya kutumia upendo huo kuwafanya wapendwa wake wahisi kupendwa. Kwa hiyo Paulo alisema,

 

Kwa maana kuishi kwangu ni Kristo, na kufa ni faida. Ikiwa nitaishi katika mwili, hiyo inamaanisha kazi yenye matunda kwangu. Hata hivyo nitakachochagua siwezi kukitambwa. Nimeshinikizwa sana kati ya hizo mbili. Nia yangu ni kuondoka na kuwa pamoja na Kristo, kwa maana hiyo ni bora zaidi.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page